Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Bi Zuhura Yunus akitoa moja ya tuzo kwa wafanyakazi wa kampuni ya Barrick kwenye hafla hiyo
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Bi. Mary Maganga akikabidhi tuzo kwa Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Zonnastraal Mumbi kwenye hafla hiyo
Waziri wa Nchini Ofisi ya Waziri Mkuu , (Ajira, Kazi na watu wenye ulemavu) Ridhiwani Kikwete akikabidhi tuzo kwa Mrakibu wa Usalama Mgodi wa Barrick North Mara , Meshack Issack
Waziri wa Nchini Ofisi ya Waziri Mkuu , (Ajira, Kazi na watu wenye ulemavu) Ridhiwani Kikwete akikabidhi tuzo kwa Mrakibu wa Usalama Mgodi wa Barrick North Mara , Meshack Issack
Wafanyakazi wa Barrick wakifurahia ushindi katika hafla hiyo
Wafanyakazi wa Barrick wakifurahia ushindi katika hafla hiyo
Waziri wa Nchini Ofisi ya Waziri Mkuu , (Ajira, Kazi na watu wenye ulemavu) Ridhiwani Kikwete akikabidhi tuzo kwa Mrakibu wa Usalama Mgodi wa Barrick North Mara , Meshack Issack
Wafanyakazi wa Barrick wakifurahia tuzo hizo
Barrick Tanzania yenye ubia na serikali kupitia kampuni ya Twiga imenyakua tuzo tano za kimkakati katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) ya 2025 iliyofanyika mjini Singida ambapo Mgodi wa Barrick Bulyanhulu umeshinda tuzo kubwa ya mshindi wa juu wa jumla katika kipengele cha Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) na Mgodi wa North Mara kuwa mshiriki bora wa maonesho ya mwaka huu (Overall Best OHS Exhibitor- North Mara).
Mbali na ushindi huo mkubwa migodi ya Barrick nchini ya Bulyanhulu, North Mara na Buzwagi ambao upo kwenye mchakato wa kufungwa imeshinda tuzo za Ujumuishaji katika maonesho (Exhibitor and Inclusion North Mara), Shughuli za mifumo ya Uchimbaji (Mining and Quarrying North Mara), ubunifu katika maonesho (Exhibitor and Innovation -Barrick Bulyanhulu), utaalamu wa ufundi wa kisayansi (Professional and Technical Scientific Buzwagi), na tuzo ya uwezeshaji wa maonesho.
Katika Hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchini Ofisi ya Waziri Mkuu (Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu) Mhe, Ridhiwani Kikwete ambaye amesisitiza umuhimu wa waajiri na wafanyakazi kuzingati sheria, kanuni na miongozo inayotolewa na serikali kupitia Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) ili kumlinda mfanyakazi na uwekezaji na biashara kwa ujumla.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa kazi (OSHA), Bi Khadija Mwenda ametumia nafasi hiyo kuwashukuru washiriki wote, waajiri na wafanyakazi kwa kuendelea kuzingatia kanuni na sheria za afya na usalama mahali pa kazi kama injini ya kuongeza uzalishaji kwenye maeneo yao ya kazi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchini kwa ujumla.
Mwakilishi wa Barrick katika hafla hiyo ambaye ni Mrakibu wa Usalama , Mgodi wa North Mara Bw. Meshack Issack amesema Barrick -Twiga itaendelea kushirikiana na serikali katika kulinda afya za wafanyakazi wake pamoja na kudumisha usalama kama nyenzo ya kuchochea uzalishaji , ufanisi na matumizi ya akili mnemba katika sekta ya madini hapa nchini.
Ushindi wa mwaka huu ni mwendelezo wa ushindi katika maonyesho ya OSHA yaliyofanyika katika miaka ya karibuni ambapo mwaka jana pia kampuni ilishinda tuzo tano ikiwemo tuzo ya mshindi wa jumla.
Suala la Afya na Usalama ni DNA ya kampuni ya Barrick na imeendelea kuwekeza katika teknolojia za kisasa za kidigitali na akili mnemba kuhakikisha inaimarisha zaidi usalama kwenye maeneo yake ya kazi na inatekeleza program za usalama ya Journey to Zero na kufanikisha kutokomeza matukio ya ajali kazini na nje ya kazi kwa wafanyakazi wake.
Mbali na kuwekeza katika usalama, Barrick imeendelea kuchangia pato la Serikali kupitia kodi na tozo mbalimbali, Kutekeleza miradi mikubwa ya kijamii kupitia fedha za CSR zinazotolewa na migodi yake hususani katika mikoa ya Mara ulipo mgodi wa North Mara na Shinyanga na Geita ulipo mgodi wa Barrick Bulyanhulu hususani katika sekta za afya, elimu na miundombinu ambayo imebadilisha maisha ya Wananchi kuwa bora zaidi.
Pia kampuni imekuwa kinara wa kutekeleza sera ya Maudhui ya ndani (Local content) ambayo inaendelea kuwanufaisha wazawa kwa kufanya kazi na migodi yake.








0 comments:
Post a Comment