Friday, 10 December 2021

AJALI YA LORI YAUA WATU ZAIDI YA WATU 53

...

Takriban watu 53 wamefariki na makumi wengine kujeruhiwa baada ya lori walilokuwa wakisafiria kupata ajali mbaya kusini mwa Mexico , mamlaka imesema.

Takriban watu 100, wanaodaiwa kuwa wahamiaji kutoka Marekani ya kati walikuwa ndani ya lori hilo wakati lilipopindukia na kugonga daraja katika jimbo la Chiapas.


Picha kutoka eneo la ajali zinaonesha waathiriwa wakiwa wametapakaa barabarani karibu na lori hilo lililopindukia.


Pia kulikuwa na miili iliopangwa ardhini ikiwa imefunikwa nguo nyeupe.


''Ni mojawapo ya ajli mbaya zaidi kutokea nchini Mexico , huku watu wengine 58 wakiwa wamejeruhiwa , wengine wakiwa na majereha mabaya'', alisema Luis Manuel Garcia , mkuu wa kitengo cha utetezi wa raia wa Chiapas.


Alisema kwamba waathiriwa walikuwa pamoja na wanaume, wanawake, na watoto. Uraia wao haujathibitishwa , lakini maafisa wa eneo hilo wanasema kwamba wengi wa waliokuwa ndani ya lori hilo ni wahamiaji kutoka mataifa ya Honduras na Guatemala.


Lori hilo liliripotiwa kuendeshwa kwa kasi kabla ya kupoteza mwelekeo katika kona na kugonga daraja la raia katika barabara kuu inayoelekea katika mji mkuu wa jimbo la Chiapas , Tuxtla Gutierrez.


Chiapas , ambalo ni jimbo linalopakana na Guatemala , ni kituo cha wahamaji wengi wasio na vibali wanaoelekea Marekani.



Mamia ya maelfu ya wahamiaji wanaotoroka umasikini na ghasia Marekani ya kati hujaribu kuvuka kupitia Mexico kila mwaka kwa lengo la kuwasili Marekani.


Wengi wao hulipa watu wanaofanya magendo , ambao huwasafirisha kinyume cha sheria wakiwa wamejazana katika malori hatari katika safari hiyo ya muda mrefu.


Mpaka wa Marekani na Mexico ni mojawapo ya mipaka hatari zaidi duniani kulingana na data kutoka kwa shirika la wahamiaji duniani IOM.


Mwaka huu pekee takriban watu 650 wamefariki katika mpaka huo, wakijaribu kuvuka , ikiwa ni zaidi ya mwaka wowote ule tangu IOM ilipoanza kuweka rekodi zake.


Pia kuna vifo vingi katika safari hiyo hatari kuelekea mpakani , hatahivyo, vifo hivyo ni vigumu kuvirekodi, ilisema IOM katika taarifa yake.


Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador alielezea ajali hiyo kuwa ya uchungu na kuandika katika twitter kwamba 'anajutia ajali hiyo'.

CHANZO- BBC SWAHILI
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger