Monday 20 December 2021

JESSE KWAYU AWASHAURI WAANDISHI WA HABARI KUUNGANA NA KUWA KITU KIMOJA KUPAMBANIA MASLAHI YAO

...

Mhariri Mwandamizi kutoka kampuni ya Media Brain Jesse Kwayu akizungumza wakati wa semina kwa waandishi wa habari mkoani Tabora iliyoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA TANZANIA) kwa ushirikiano wa International Media Support (IMS)
Mhariri Mwandamizi kutoka kampuni ya Media Brain Jesse Kwayu akizungumza wakati wa semina kwa waandishi wa habari mkoani Tabora iliyoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA TANZANIA) kwa ushirikiano wa International Media Support (IMS)
Waandishi wa habari nchini wameshauriwa kuungana na kuwa kitu kimoja ili wawe na nguvu ya kupambania maslahi yao pamoja na kudai mabadiliko ya vifungu mbalimbali vya sheria ambavyo vinaonekana kuminya utendaji wa wana habari na vyombo vya habari nchini.

Rai hiyo imetolewa na Mhariri Mwandamizi kutoka kampuni ya Media Brain Jesse Kwayu wakati akiwasilisha mada katika semina ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Tabora iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Akizungumza katika semina hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA TANZANIA) kwa ushirikiano wa International Media Support (IMS),Kwayu amewataka Waandishi kutoka makundi mbalimbali kuwa kitu kimoja ili kuwa na nguvu na sauti ya kupaza katika mambo muhimu na changamoto zinazoikabili tasnia hiyo.

"Tumeona huko siku za nyuma kipindi ambacho zinapitishwa sheria hizi zinalalamikiwa leo,Waandishi tuligawanyika hivyo ikawa rahisi sana kwa yale ambayo yanaonekana ni mapungufu maana ndani yetu wapo walioyakubali",amefafanua.

Kwayu ameongeza kwamba kundi lolote linapogawanyika linakuwa halina nguvu ya kusimamia mambo yake hivyo litaishia kutawaliwa kutawaliwa kutokana na kugawanyika huko ambalo mara nyingi hutokea kwa makusudi ya watawala (divide and rule).

Pamoja na hilo Kwayu amewataka Waandishi hao kuzisoma na kuelewa vifungu mbambali vya sheria zilizopo nchini ili kuweza kufanya kazi zao kulingana na uhitaji wa sheria hizo.
"Sekta ya habari Tanzania inasimamiwa na sheria nyingi,ni wajibu wa kila mwandishi kuzisoma ili ziwasaidia katika kazi yenu ya kukusanya na kuchakata habari", amesema.

Kwa upande wake mshiriki wa semina hiyo Joseph Ndau ambaye pia ni mwakilishi wa EFM/TVE mkoani Tabora amekiri uwepo wa makundi miongoni mwa wana habari kutokana na mbalimbali ikiwemo elimu,ukubwa wa vyombo na hali za maisha.

Ndau amesema wapo Waandishi wenye elimu wanawadharau wasio na elimu na wapo wanaofanya kazi katika vyombo vikubwa wanawadharau waliopo kwenye vyombo vinavyoonekana ni vidogo.
"Kuna haja ya Waandishi kuondoa makundi miongoni mwetu,tuwe kitu kimoja ili tuwe na sauti moja na yenye nguvu katika kushiriki wa mijadala mbalimbali hususani ile utungwaji au mabadiliko ya sheria za habari." amesisitiza.

Naye mshiriki Orpa Zephania ameshauri taasisi mbalimbali zinazosimamia tasnia ya habari kuandaa mijadala ya mara kwa mara hususani kwa Waandishi waliopo mikoani ili kujenga uelewa wa sheria hizo kwa Waandishi hao.

"Tunawashukuru MISA Tanzania kwa kutukumbuka waandishi wa Tabora,semina kama hizi zinatakiwa zifanyike mara kwa mar ili kuwajengea uwezo na ujasiri Waandishi wa kufanya kazi zao." amesema.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Waashiriki, mwandishi mwandamizi mkoani Tabora Robert Kakwesi amewashukuru MISA TANZANIA kuandaa semina hiyo mkoani hapo na kuahidi kufanya kazi kwa vitendo yale waliyokubaliana (resolutions).
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger