Mtendaji Mkuu mpya wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro N. Kilahala kulia akipokea baadhi ya nyaraka za makabidhiano kutoka kwa Bi. Monica A. Moshi ambaye alikuwa ameshikilia ofisi hiyo kwa muda. Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya Wakala wa Ufundi na Umeme zilizopo mjini Dodoma na kushuhudiwa na viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ambao walimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Mtendaji Mkuu mpya wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro N. Kilahala akitambulishwa kwa watumishi wa Wakala huo mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi kutoka kwa Bi. Monica A. Moshi ambaye alikuwa ameshikilia ofisi hiyo kwa muda. Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya Wakala wa Ufundi na Umeme zilizopo mjini Dodoma na kushuhudiwa na viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ambao walimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (DODOMA)
************************
Na. Alfred Mgweno
Lazaro N. Kilahala leo amekabidhiwa rasmi ofisi kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu aliyekuwa akishikilia ofisi hiyo kwa muda, Mkurugenzi wa Uendeshaji Bi. Monica A. Moshi. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za makao makuu ya Wakala wa Ufundi na Umeme zilizopo mjini Dodoma na kushuhudiwa na viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ambao walimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Akizungumza na watumishi wa makao makuu mara baada ya kukabidhiwa ofisi, Mtendaji Mkuu mpya amesema TEMESA ni taasisi kubwa na akaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha na watumishi wote kwani kazi nzuri imekwishafanyika huko nyuma hivyo kikubwa ni kushirikiana na kufanya kazi kwa umoja na kwa pamoja ili kuliendeleza gurudumu la maendeleo mbele.
‘’Ninafurahi sana tumeonana hapa leo,na sura zote hizi zinaonyesha matumaini makubwa sana, kwahiyo sina chembe ya shaka kwamba hizi ni sura za ushindi, basi tuibebe hiyo taswira, tuendelee kufanya kazi kwa pamoja na tuamini kwamba tunaweza, hatupo hapa kwa bahati mbaya, tupo hapa kwasababu tunastahili kuwepo na yale yaliyokusudiwa kutekelezwa na TEMESA sisi ndio tutakaoyatekeleza, sio mtu mwingine’’. Alisema Mtendaji Mkuu na kuwashukuru watumishi hao kwa kumkaribisha na kuwaomba kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa umoja.
Aidha, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Richard L. Mkumbo akizungumza na menejimenti ya Wakala huo wakati wa makabidhiano hayo, amesema Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi itakua bega kwa bega kuhakikisha gurudumu la Wakala linaendelezwa mbele na kutokurudi nyuma.
‘’Kimsingi TEMESA kuna maendeleo makubwa tu, ukisoma utaona maendeleo makubwa, karakana zinaongezeka, bajeti imeongezeka kwahiyo uchukue pale uendeleze mbele yale mazuri’’. Alisema Mwakilishi wa Katibu Mkuu.
Naye Mtendaji Mkuu aliyeshikilia kiti hicho kwa muda, Bi. Monica A. Moshi ambaye ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Wakala huo, akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ameushukuru Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA kwa kumpa ushirikiano wa kutosha kwa muda mfupi ambao ameshikilia kiti hicho na kuwaomba kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi.
0 comments:
Post a Comment