Monday 20 December 2021

MISA TANZANIA YAWAPIGA MSASA WA SHERIA WAANDISHI WA HABARI NA CSO's SHINYANGA...KWAYU ATAKA 'KELELE MADHAIFU YA SHERIA'

...
Kaimu Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Andrew Marawiti akizungumza wakati akifungua semina kwa waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu sheria mbalimbali zinazosimamia Tasnia ya Habari nchini Tanzania.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA Tanzania) ikishirikiana na International Media Support (IMS) imeendesha semina kwa waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu sheria mbalimbali zinazosimamia Tasnia ya Habari nchini Tanzania.

Akifungua Semina hiyo leo Jumatatu Desemba 20,2021 Kaimu Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Andrew Marawiti amesema ili waandishi wa habari wafanye kazi katika mazingira mazuri ni vyema wakazijua sheria zilizopo ndiyo maana MISA Tanzania imeendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari.

Marawiti amesema Sheria na Kanuni wanazopaswa kuzielewa vizuri waandishi wa habari ni pamoja na Sheria ya Huduma za Habari -2016, Sheria ya Takwimu - 2019 na Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) 2010.

“Endapo Waandishi wa Habari watazifahamu vyema Sheria na Kanuni zinazosimamia taaluma ya Habari na wataweza kutambua wajibu wao na kutimiza majukumu yao kikamilifu na wataelewa namna ya kukabiliana na changamoto zinazotokana na Sheria hizo”,amesema.

Akiwasilisha mada wakati wa semina hiyo, Mhariri Mwandamizi kutoka Kampuni ya Media Brain Jesse Kwayu amesema ni wajibu wa waandishi wa habari kuzijua sheria zinazohusu tasnia ya habari pamoja na kuzipigia kelele sheria zinazolalamikiwa kukandamiza uhuru wa habari na vyombo vya habari.

Amesema Waandishi wa Habari pamoja na wadau wengine wanapaswa kupaza sauti kuhusu madhaifu yaliyopo katika sheria zinazosimamia tasnia ya habari.

“Ni muhimu Waandishi wa habari wakawa kitu kimoja ili kuwa na nguvu na sauti ya kupaza kuzipigia kelele sheria kandamizi zirekebishwe ili ziwe rafiki kwa walio ndani na nje ya mamlaka za serikali . Tupige kelele ili sheria hizi zirekebishwe, ziwe rafiki kwa kila mtu ndani ya taifa letu”,amesema Kwayu.

“Watu wote wenye nafasi za kurekebisha sheria zinazolalamikiwa kukandamiza uhuru wa habari na vyombo vya habari wafanye kazi ya kuzirekebisha kwa maslahi ya watu wote katika taifa”,ameongeza Kwayu.

Kaimu Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Andrew Marawiti akizungumza wakati akifungua semina kwa waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu sheria mbalimbali zinazosimamia Tasnia ya Habari nchini Tanzania. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Andrew Marawiti akizungumza wakati akifungua semina kwa waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu sheria mbalimbali zinazosimamia Tasnia ya Habari.
Kaimu Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Andrew Marawiti akiwasisitiza waandishi Waandishi wa Habari kuzifahamu sheria mbalimbali zinazosimamia Tasnia ya Habari nchini Tanzania.
Mhariri Mwandamizi kutoka Kampuni ya Media Brain Jesse Kwayu akiwasilisha mada kwenye semina kwa waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga na kupaza sauti kuhusu madhaifu yaliyopo katika sheria zinazosimamia tasnia ya habari ili ziweze kurekebishwa.
Mhariri Mwandamizi kutoka Kampuni ya Media Brain Jesse Kwayu akiwasilisha mada kwenye semina kwa waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga
Mhariri Mwandamizi kutoka Kampuni ya Media Brain Jesse Kwayu akiwasilisha mada kwenye semina kwa waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga
Waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.

Waandishi Waandishi wa Habari  wakiwa ukumbini.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger