Friday 24 December 2021

WATATU WATIMKA AZAM FC, YUPO DUBE

...

JUMLA ya wachezaji watatu wanatarajiwa kuondoka katika kikosi cha Azam FC kwenda katika timu ya taifa ya Zimbabwe kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON).

Wachezaji hao ni beki wa kushoto, Bruce Kangwa, kiungo Never Tigere na mshambuliaji Prince Dube. Nyota hao huenda wakosekana katika michezo baadhi ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA kutokana na kuwepo katika majukumu ya timu ya taifa.

Kwa mujibu wa mtandao wanchi ni Zimbabwe, wachezaji hao wameitwa katika kikosi cha awali kuelekea michuanoya AFCON itakayoanza Januari 9 hadi Februari 6, 2022 nchini Cameroon.

Mastaa hao wa Azam, wanatarajiwa kuingia kambini hivi karibuni kwa ajili ya mchujo wa mwisho utakaowawezesha kuwepo sehemu ya kikosi cha Zimbabwe kitakachokwenda Cameroon katika michuano
hiyo.

Ofisa Habari wa Azam FC, Thabiti Zakaria, alithibitisha hilo kwa kusema: “Ni kweli wachezaji hao wameitwa katika kikosi cha awali cha timu ya taifa ya Zaimbabwe, hivyo muda wowote watajiunga nayo.”
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger