Wednesday, 26 August 2020

Tundu Lissu Ashindwa Kufika Mahakamani....Kesi Yapigwa Kalenda

...
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia (CHADEMA), Tundu Lissu ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu anapokabiliwa na kesi ya uchochezi kwa sababu ya kukwamishwa na mchakato wa kurudisha fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Lissu alitarajiwa kufika mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kassian Matembele kwa ajili ya mwenendo wa kesi yake ya uchochezi.

Wakili wa Lissu, Peter Kibatala amesema kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na NEC, Lissu na mgombea wake Mwenza walitakiwa kurudisha fomu za kugombea urais na kupatiwa za uteuzi saa 6 mchana kisha aanze safari za kurejea Dar es Salaam kuhudhuria kesi zake.

Amesema kwa bahati mbaya mpaka saa 2:30 usiku wagombea hao walikuwa awajatoka katika ofisi za tume hivyo kusababisha ratiba zake za usafiri kurejea Dar es Salaam kuharibika.

“Hivyo naiomba mahakama iridhie kuahirisha kesi hii na kupanga tarehe nyingine ambayo naamini mshtakiwa atakuwepo mahakamani,”  Kibatala

Baada ya Kibatala kueleza hayo, Wakili wa Serikali Mkuu Renatus Mkude amedai kuwa kwa mazingira hayo yaliyoelezwa na Wakili wa Utetezi hawana pingamizi hivyo rai yao shauri hilo liahirishwe hadi tarehe nyingine.

Hakimu Mkazi Mwandamizi Kassian Matembele ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 24, mwaka huu.

Katika kesi hiyo namba 123 ya mwaka 2017, Lissu anadaiwa kutoa maeneno ya uchochezi wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Deman, Zanzibar, Januari 11, 2017, akiwa eneo la Kibunju Maungani, Wilaya ya Magharibi B, mkoni Mjini Magharibi.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger