Friday 28 August 2020

Rais wa Uganda Yoweri Museveni atangaza siku ya kitaifa ya maombi kwa ajili ya Corona nchini Humo

...
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza siku ya kitaifa ya maombi kwa ajili ya Covid-19 itakayofanyika jumamosi Agosti 29, 2020.

Amesema wazo lakufanya hivyo amelipata kutoka kwa raia wa Uganda ambaye alikuwa na 'Maono kutoka kwa Mungu'.

"Kuna Mtu amenifuata na kuniambia Mungu kamuambia kwenye maono kwamba ninapaswa kuandaa maombi ya kitaifa ili Mungu atuepushe na corona, kwahiyo natangaza kuwa Aug 29,2020 ni siku ya maombi ya Kitaifa na pia itakuwa siku ya mapumziko, baki nyumbani kwako na uombe”" Museveni amesema katika ujumbe wake wa mtandao wa kijamii.

Hadi sasa Uganda imerekodi watu 2,679 wenye maambukizi ya virusi vya coronana na  vifo 28.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger