Monday 31 August 2020

Mtoto darasa la pili, miaka (9) mkoani Kigoma alipukiwa na bomu

...
(Picha:Mtandao)
Mtoto mwenye mwenye umri wa miaka 9 katika kijiji cha Kasumo kata ya Kajana wilayani Buhigwe mkoani Kigoma amepoteza maisha baada ya kulipukiwa na bomu Agosti 28, 2020.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi James Manyama amesema,''Mtoto huyo ajulikanaye kwa jina la Abas Jeras, mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Lemba kijiji cha Kasumo Kata ya Kajana alipatwa na mkasa huo tarehe 28 mwezi wa nane mwaka huu baada ya kuokota bomu bila kujua na kuanza kulichezea kisha bomu hilo kulipuka na kusababisha apoteze maisha''.

Polisi inahusisha uwepo wa bomu hilo katika kijiji hicho huenda ni kilikuwa likitumiwa kama njia na makundi ya waasi waliokuwa wakitoka nchi ya Burundi kwenda kambi ya wakimbizi ya Mtabila hivyo kudhaniwa huenda liliangushwa na watu hao.

Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi wote wanaoishi vijiji vinavyopakana na nchi ya Burundi kuwakataza watoto kuokota vitu na kuvichezea ili kuepusha madhara kama yaliyotokea.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger