Saturday 29 August 2020

UWANJA WA JAMHURI DODOM KUMEANZA KUNOGA MAPEMA...CCM WANA JAMBO LAO

...

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

KUMEANZA  kunoga mapema Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma!Ndivyo unavyoweza kuelezea jinsi ambavyo idadi kubwa ya wananchi wakiwemo wana CCM ambavyo wamejitokeza uwanjani hapo kushuhudia uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi Dk.John Magufuli.

Ratiba inaonyesha wananchi walianza kuingia uwanjani saa 12 asubuh. Lakini hadi saa tatu uwanja ulishaanza kufurika kuanzia majukwaa yote na katikati ya uwanja vikundi mbalimbali vilionekana wakipiga jaramba huku wengine wakiendelea kuingia uwanjani hapo.

Hali  hiyo pengine haikufikiriwa kwa kuwa wasanii walipoanza kutumbuiza saa mbili asubuh tayari mashabiki wao(wananchi)walikuwa tayari kuwashangilia kinyume na matarajio pengine uwanja ungefurika nyakati za mchana.

Aidha, ni dhahiri wanaCCM pamoja na wananchi wengine wasio makada wa chama hicho hawakutaka kuwa sehemu ya wale watakaohadithiwa au kuangalia kwenye runinga na mitandao ya kijamii kile kitakachotokea Uwanja wa Jamahuri.

Michuzi TV na Michuzi Blog imeshuhudia msusuru wa umati mkubwa wa wananchi ukiendelea kuingia uwanjani hapo huku wale ambao wameshafika uwanjani wakiendelea kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya,wanamuziki wa dansi, waigizaji na kila aina ya wasanii kuhakikisha kila aina ya burudani inapatikana.

Hata hivyo wakati wananchi hao wa Jiji la Dodoma pamoja na Wana CCM hao wakiendelea kupata buradani za nguvu ambazo kwa lugha ya mjini wanaita burudani Konki wapo wananchi wengine ambao wameonekana kuwa makini wakisoma majarida,vipeperushi pamoja na gazeti la Uhuru ambalo ni gazeti la Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambayo yanaelezea maendeleo na mafanikio makubwa ambayo Serikali ya Awanu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli imeyapata katika miaka mitano ya kwanza.

Aidha, uelewa mpana wa wananchi kuhusu  mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Magufuli kipenzi cha Watanzani imekuwa karata ya turufu kwa CCM wakati wakianza kampei zao leo jijini Dodoma ambako pia ndio makao makuu ya nchi na chama hicho.

Ukweli kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Serikali itamsaidia kwa kiasi kikubwa mgombea wa CCM kunadi Ilani ya Chama chao kwa urahisi na kuongeza mawili matatu bila ya kutumia nguvu nyingi kuongeza ahadi.





Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger