Mgombea Urais wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba amemshukia vikali mgombea Urais wa CHADEMA Tundu Lissu baada ya kumuwekea pingamizi tume ya Taifa ya Uchaguzi ili jina lake lienguliwe.
Profesa Lipumba, amesema wananchi na wanachama wa chama hicho walipata taharuki baada ya kuona kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii taarifa za kuwekewa pingamizi na mgombea urais wa CHADEMA, Lissu.
Profesa Lipumba, amesema wananchi na wanachama wa chama hicho walipata taharuki baada ya kuona kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii taarifa za kuwekewa pingamizi na mgombea urais wa CHADEMA, Lissu.
Amesema kuna hoja nzito za kuzungumza kwenye jamii kuelekea uchaguzi mkuu na si kuleta hoja za kuleta mapingamizi ambazo hazina mashiko kwa Taifa.
Alifafanua kwamba alishangazwa na hoja ya Lissu kwenye pingamizi alilotoa wakati chama chake kilifuata maelekezo ya NEC.
“Nakuongeza Lissu ni mwanasheria mbobezi, lakini anatoa hoja dhaifu kwenye pingamizi lake, nawaomba wana-CHADEMA wamsaidie, kwani inawezekana anaomba huruma ya wananchi ili wamchague kutokana na changamoto aliyokutana nayo,”amesema Profesa Lipumba na kuongeza;
“Mbona mgombea wa ACT-Wazalendo, Bernard Membe ambaye amerudisha fomu kwa sheria hizi hizi hawajamuwekea pingamizi? Wanajua kwamba Profesa Lipumba ni mti wa mpingo na anahoja za msingi kuelekea uchaguzi mkuu.
Leo CHADEMA na Lissu wanazuia Uhuru wa wananchi wa kupiga kura kwa mgombea wanayemtaka kwa kuweka pingamizi ambalo halina mashiko, lakini niwatoe hofu wanachama na Watanzania kwamba CUF imejipanga na tunakwenda kupeleka Sera nzito kwa ajili kuleta furaha kwa Watanzania.”
Profesa Lipumba amesema baada ya kupata taarifa za pingamizi hilo wao kama chama walishaweka kila kitu sawa na wamewaondoa hofu Watanzania kwamba watashiriki uchaguzi kama kawaida na mapema watatangaza kuanza kwa kampeni.
Mwanasheria wa CUF, Salvatory Magafu, amesema changamoto iliyojitokeza kwa Lissu ni kwa sababu kabla ya kufikia mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu NEC walikutana na vyama vya siasa na wakashauriana na kukubaliana mambo mbalimbali na kwa bahati mbaya Lissu alikuwa nje ya
nchi.
0 comments:
Post a Comment