Monday, 31 August 2020

Waandishi wa Habari Waaswa kutoa elimu kwa umma kuhusiana na magonjwa ya mlipuko

...
Samira Yusuph
Simiyu.
Waandishi wa habari mkoani Simiyu wameaswa kutoa elimu kwa umma kuhusiana na magonjwa ya mlipuko ili kuongeza uelewa wa namna ya kujikinga na kukabiliana na magonjwa hayo kwa jamii.

Akiwafunda waandishi wa habari, Mratibu wa magonjwa ya mlipuko mkoani Simiyu Dk Hamis Kulemba amewataka waandishi wa habari kuwa kioo katika kutoa elimu ya magonjwa ya mlipuko ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa.

"Mkawe mabalozi wazuri kwa wananchi kwa sababu nyinyi mpo karibu na wananchi na mnaishi nao hivyo tumieni nafasi hiyo kuhakikisha kuwa elimu inafika kwa wananchi na wanaitumia ipasavyo," alisema Kulemba.

Aidha kulemba alisema kuwa kinga kubwa ya magonjwa ya mlipuko ni usafi hivyo wananchi wakielimishwa kuhusu usafi wa mazingira yao itakuwa ni msaada ambao ni kinga na utaleta manufaa katika jamii.

Akifafanua namna ambavyo wamekuwa wakikumbana na changamoto ya magonjwa ya mlipuko Dr Nyangi Thomas alisema kuwa katika mkoa huu ugonjwa mkubwa unaosumbua ni kuhara.

"Kumekuwa na namba kubwa ya wagonjwa wa kuhara hasa watoto na hii inatokana na hali ya mazingira ya huko vijijini inakuwa ni changamoto kukabiliana nayo sisi wakija hapa wanapata huduma lakini tunawapa elimu pia ili wakirudi vijijini wakafunfishane namna ya kujikinga," alisema Dr Nyangi.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa wa mitaa ya bariadi wameeleza ufahamu wao kuhusiana na kujikinga na magonjwa ya mlipuko na kusisitiza kuwa elimu inahitajika zaidi katika jamii ili waweze kujilinda dhidi ya magonjwa hayo.

"Kidogo afadhari saizi baada ya mlipuko wa ugonjwa wa kovid-19 uelewa umeongezeka kwenye kunawa mikono na kuwa wasafi lakini bado kuna yale mazoea ndio yanatutesa inabidi tuelimishwe zaidi," alisema Raheri George mkazi wa Kidinda.

"Yaani mambo ya kunawa mikono tumeanza kuyasahau saizi, lakini ni vizuri sana kama tukiyazingatia kwa sababu ilikuwa ni vizuri na tuliepuka hata  virusi vya korona wapite hata na matangazo ili kutukumbusha tusijisahau,"alisema Zainabu Banemhi mkazi wa Bariadi.

Katika maeneo mengi ya kanda ya ziwa ugonjwa wa kuhara umekuwa ukishika kasi kutokana na hali halisi ya mazingira ya mazoea ambapo asilimia kubwa ya wakazi wake ni wakulima, wavuvi na wafugaji.

Mwisho.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger