Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Harry Kitilya, Shose Sinare, Sioi Solomon, Bedason Shallanda na Alfred Misana wamekiri makosa na wametakiwa kulipa TZS 1.5 bilioni kama fidia kwa kuisababishia hasara Serikali na kila mmoja kulipa faini shilingi milioni 1 ya mahakama au kwenda jela miezi sita, kutokana na kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabiri
Mashtaka yote 58 yalifutwa na kubakiza shtaka moja la kuisababishia hasara serikali. Kesi hii ilianza jana saa 11 na kuisha saa 2 usiku katika Mahakama ya Mafisadi.
Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani milioni 550 kwa Serikali ya Tanzania kutoka benki ya Standard ya Uingereza.
Aidha, wanadaiwa kula njama za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ili waweze kujinufaisha wenyewe na washirika wao. Mawakili wa washtakiwa walikuwa ni Alex Mgongolwa na Jeremiah Mtobesya.
0 comments:
Post a Comment