Friday, 21 August 2020

NEC yatoa siku 2 kwa Vyama vilivyopata changamoto kutambulisha Wagombea wao baada ya Watu wasioteuliwa kuchukua fomu za Uteuzi

...
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema inafuatilia zoezi la kuchukua fomu za uteuzi na kubaini kuwa kuna changamoto ambazo zimejitokeza kutokana na vyama vya siasa kutokujipanga na kuweka utaratibu mzuri wa Wagombea wao kuchukua fomu za Utezi

Tume imesema kutokana na hilo watu ambao hawakuteuliwa na vyama vyao wamejitokeza na kwenda kuchukua fomu za uteuzi za kugombea Ubunge au Udiwani bila ridhaa ya vyama husika na kupelekea walioteuliwa kushindwa kuchukua fomu

Kwa mujibu wa Tume hiyo Majimbo yaliyoathirika ni Kibamba, Mbagala, Kilombero, na Kigamboni

Hivyo, Tume imetoa nafasi kwa vyama vya siasa kuwatambulisha Wagombea wao kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ndani ya siku 2 kuanzia Agosti 20, 2020 kwa majimbo na Kata zilizo na changamoto


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger