Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limefanikiwa kuwakamata watu kumi (10) wanaojihusisha na usajili line za simu kwa kutumia vitambulisho vya watu wengine na kuzalisha line nyingi kwa kitambulisho kimoja bila ridhaa ya mwenye kitambulisho.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema kuwa line hizo wamekuwa wakiuuza kwa wa halifu na watu wasio na vitambulisho ambao ni wahalifu.
Aidha muroto ameongeza kuwa wamewakamata wahamiaji wahamiaji haramu wanne ambao ni raia wa Ethiopia huku akisema raia hao wanne walikamatwa katika eneo la chipolo wilayani mpwapwa wakiwa wanasafirishwa katika basi Namba T.112 ATC SCANIA Bus la Kampuni ya Premere line linalofanya safari kutoka mwanza kwenda mbeya.
Hatahivyo, kamanda muroto amesema kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa yote wameanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi ambavyo sasa wanasaidia jeshi la polisi kuwaibua wahalifu wote katika mitaa yao wanaohifadhi wahalifu pamoja na wapokeaji wa mali zinazotokana na uhalifu.
Katika hatua nyingine kamanda muroto amewataka Madereva kuheshimu sheria za usalama barabarani huku akisema kuwa anayetembea kwa miguu ana haki ya kisheria kama dereva anaye endesha barabarani.
Methew Benjamini ni Mrakibu msaidizi,wa jeshi la polisi, Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Dodoma amesema wameamua kujikita katika utoaji wa elimu zaidi ya usalama barabarani hasa katika vivuko vya waenda kwa miguu ambapo zaidi ya asilimia 76 ya ajali za barabarani hapa nchini husababishwa na makosa ya kibinadamuikiwa ni pamojana uzembe wa madereva.

Nao watembea kwa miguu wamesema kuwa walikuwa hawana elimu ya kutosha juu ya vivuko hivyo vya watembea kwa miguu huku wengine wakitoa ushauri kwa madereva kufuata sheria za barabarani
0 comments:
Post a Comment