Sunday 30 June 2019

Katibu Mkuu Wizara Ya Afya Azindua Baraza La Wafanyakazi Hospital Ya Benjamin

...
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya  Benjamin mkapa imefungua na kuzindua Baraza jipya la wafanyakazi  tangu hospitali ianzishwe  ambayo ni miongoni mwa hospitali kubwa hapa nchini. 

Akizungumza katika uzinduzi  huo,na wafanyakazi  wa Baraza la wafanyakazi Hospitali ya Rufaa Benjamin Mkapa iliyopo jijini Dodoma,katibu mkuu Wizara  ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dokta.Zainab Chaula ametoa rai kwa Wafanyakazi  wa baraza hilo kuwajibika katika Kazi zao na kufanya kazi kwa kujituma zaidi na kuonesha uzalendo kwa Wagonjwa. 

Dokta Chaula amesema kazi ya Utabibu na Udaktari ni ya  neema  na Rehema kutoka  kwa Mwenyezi Mungu na inayohitaji kuwa na uvumilivu , huruma na maneno ya Faraja kwa Wagonjwa hivyo kila  Mmoja anatakiwa kuguswa pindi anapotoa huduma kwa mgonjwa. 

“Tunajifunza kila siku,kwa hiyo nyie mlioteuliwa mtuwezeshe,haki haipo bila wajibu,na kila mmoja akijituma atatimiza wajibu  wake,mimi sikumbuki kutumwa na napata shida kum-push  mtu,na lazima tutengeneze Mechanism ya watu kufanyakazi bila kutumwa.Hakuna kazi  ya   neema na ibaada tunayo fanya kama hii,Mtu ana Stress zake,ana shida,hana hela lakini unamfariji,unamtibu,mwisho wa kazi saa 9 ukifanya kazi mpaka saa 11 au saa 1 jioni una dhambi gani.”Alisema. 

Aidha ,Dokta Chaula amewataka wafanyakazi kuwa Wepesi katika kutekeleza Majukumu yao na kutowakwaza wagonjwa na wananchi kwa ujumla hivyo ni jambo la busara kupeana Moyo katika kazi ngumu na yenye wito ya  utabibu na kumtegemea Mungu katika changamoto wanazokumbana nazo . 

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Afya  Dokta Chaula amesema upendo na huruma ni jambo la Muhimu kwa Maisha ya Binadamu kwani ni Moja ya Kujenga Marafiki wengi  na kusema kuwa hakuna mtu mdogo katika maisha kila mtu ana  mchango wake na kinachotofautisha ni Madaraka na Mamlaka tu ila  binadamu wote ni sawa.. 

“Kwa makusudi tu mtu anakuja  halafu anatoka analia  ofisini kwako unajisikiaje,lazima tupendane tuhurumiane tukitengeneza system ya namna hii katika maisha yetu tutakuwa na marafiki wengi kuliko maadui,tusameheane”Alisema. 

Kwa upande wake Katibu wa Baraza la wafanyakazi mkoa wa Dodoma,ambaye pia Mjumbe Taifa wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali kanisa  la Waadventista Wasabato ,[ATAPE] Bw.Mchenya John  amesema amesema wataendelea kuyafanyia kazi maelekezo yote  muhimu yaliyotolewa huku akizungumzia namna  walivyofanya mchakato wa   uanzishaji wa Chuo wa Chuo kikuu cha Dodoma pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa akitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa awamu ya nne Dokta.Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufanikisha uanzishaji  wa Hospitali hiyo. 

Naye Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi  Taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa ambaye pia mkurugenzi mtendaji wa Hospitali hiyo Dokta Alphonce Chandika  amesema taasisi hiyo ina takriban  miaka mitatu tangu ianzishwe na walikuwa hawajaunda Baraza la Wafanyakazi kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wafanyakazi lakini kwa sasa idadi imejitosheleza na wameona kuwa na umuhimu wa kuwa na Baraza ambapo tayari na  katiba na mkataba wa Baraza hilo ilishatengenezwa.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger