NA SALVATORY NTANDU
Abiria saba Wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamenusurika kifo baada lori la mizigo aina ya Fuso lenye T 322 ACC walilokuwa wakisafiria kugongana na basi aina ya Scania lenye namba za usajili T 245 AJS Kwela Classic Mali ya Laurent Ncheye mkazi wa Kahama linalofanya safari za kahama kwenda mkoani Kigoma.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanya Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ajali hiyo leo asubuhi baada ya dereva wa basi hilo kuligonga lori hilo lilokuwa limebeba magunia 100 ya mahindi katika eneo hilo na kusababisha lori hilo kupinduka na kusababisha majeruhi wa ajali hiyo.
Amesema majeruhi hao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Halmashauri ya mji wa Kahama na hali zao zinaendelea vizuri na kuwataka madereva wote wilayani humu kuheshimu alama za barabarani husasni wanapotaka kuingia katika makutano ya barabara ili kuzuia ajali zinazoweza kuzuilika.
Kamanda Abwao amesema chanzo cha ajali hiyo ni Uzembe wa Dereva wa basi hilo kutochukua tahadhari pindi anapongia katika makutano ya barabara kwa kuingia katika barabara hiyo kwa mwendo kasi na kusababisha ajali hiyo ambayo imeharibu miundo mbinu ya barabara na nyumba za watu zilizopo karibu na eneo hilo.
Amefafanua kuwa dereva wa basi hilo amejisalimisha katika kituo cha polisi kahama na baada ya kuhojiwa atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinayomkabili.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama DK, George Masasi amesema amepokea majeruhi hao Saba na hali zao zinaendelea vizuri ambao ni pamoja na dereva wa lori hilo ambao wameumia katika sehemu mbalimbali za miili yao.
Mmoja wa shuhuda wa Tukio hilo Amosi Joseph amesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 11 alfajiri baada ya dereva wa basi kupita katika eneo hilo kwa mwendo kasi kwa lengo la kuwahi abiria katika kituo kikuu cha mabasi kahama kwaajili ya kuanza safari na kusababisha abiria waliokuwepo katika lori hilo kujeruhiwa.
Mbali na Kamanda Abwao amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuchukua hatua kali kwa madereva wote wazembe ambao hawazingatii sheria za usalama barabarani .
0 comments:
Post a Comment