Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Cameroon Joel Tagueu hatoshiriki katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu kutokana na matatizo ya moyo.
Picha aliyopigwa wakati wa mazoezi ya timu hiyo ya Indomitable Lions huko Qatar ziligundua tatizo katika mshipa wa moyo wa mshambuliaji huyo.
Taarifa katika mtandao wa shirikisho la soka nchini humo inasema hakuna "hakikisho la kuondosha hatari kwa mchezaji huyo kufariki ghafla uwanjani".
Kocha mkuu Clarence Seedorf anatarajiwa kuita mchezaji za ziada kuichukuwa nafasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
Kwa mujibu wa daktari wa kikosi hicho Prof William Ngatchou, Tagueu, aliyeichezea timu ya Ureno Maritimo, msimu uliopita amekuwa akifanyiwa ukaguzi sawa na huo na alipigwa picha kwa takriban miaka minane lakini matokeo yalishindwa kudhihirisha matatizo yoyote.
Kikosi cha Cameroon kinashuka dimbani leo dhidi ya Guinea Bissau leo katika mashindano hayoya kombe la mataifa ya Afrika mwendo wa saa mbili usiku saa ya Afrika mashariki.
0 comments:
Post a Comment