MAHAKAMA
ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara imemhukumu, Ally Mpemba au Ustadhi
(32), Mkazi wa Mtaa wa Bunda Stoo mjini Bunda kifungo cha miaka 60 jela
baada ya kupatikana na hatia ya kubaka watoto wawili kwa zamu akijifanya
polisi.
Adhabu
hiyo ilitolewa juzi na Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Bunda, Said
Kasonso, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo
pasipo kuacha shaka yoyote.
Awali
ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Hamuza
Mdogwa, kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Januari 17 mwaka
huu, majira ya saa 8:30 mchana, katika kijiji cha Kitaramanka wilayani
hapa.
Alisema
kuwa mshtakiwa huyo aliwakuta watoto hao wakiwa katika eneo hilo na
akawatisha kuwakamata akidai kuwa yeye ni askari Polisi na kwamba
wamefanya kosa hivyo atawachukua maelezo yao na baadaye awapeleke
kituoni.
Aliongeza
kuwa mshtakiwa huyo alitoa Sh 200 na kumpatia mtoto mmoja aende
akanunue daftari la kuandikia maelezo yao, na baada ya mtoto huyo kwenda
ndipo alipombaka aliyebaki na kisha kumwambia adhabu yake imekwisha
sasa aende nyumbani.
Alisema
kuwa baada ya yule aliyetumwa daftari kurudi, Mpemba alimbaka pia na
kumuamuru arudi nyumbani adhabu yake imekwisha na kwamba watoto hao
baada ya kufanyiwa unyama huo walikwenda kutoa taarifa nyumbani kwa
wazazi wao.
Aidha
alisema kuwa Ofisa Mtendaji wa kata hiyo kwa kushirikiana na wananchi
wa kijiji hicho walimkamata mshtakiwa huyo na kumfikisha Polisi.
Kabla ya adhabu kutolewa mshtakiwa huyo alipewa fursa ya kujitetea na akaiomba Mahakama hiyo impunguzie adhabu.
Hata
hivyo mwendesha mashitaka huyo aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali
kwa mshtakiwa huyo kwa sababu makosa aliyofanya ni ya kinyama na ya
udhalilishaji mkubwa kwa watoto hao wenye umri wa miaka 16 kila mmoja.
Akitoa
hukumu hiyo, Hakimu Kasonso, alisema kuwa ameridhika na ushahidi
uliotolewa mahakamani hapo na kwamba kwa kosa la kwanza la kubaka mtoto
wa kwanza ataenda jela miaka miaka 30 na la pili pia atatumikia kifungo
cha miaka 30 jela na adhabu zote zinakwenda kwa pamoja hivyo atatumikia
kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine
wenye nia na tabia kama hiyo.
0 comments:
Post a Comment