Friday 3 April 2015

Breaking News!! MASHABIKI WA SIMBA WAFARIKI AJALINI WAKIENDA SHINYANGA KUSHUHUDIA MCHEZO KATI YA KAGERA SUGAR vs SIMBA SC

...
Basi ndogo aina ya coaster lililokuwa likitokea jijini
Dar es Salaam kuelekea Shinyanga limepata ajali eneo la Makunganya barabara kuu ya Dodoma-Morogoro na kusababisha watu watano kufariki dunia papo hapo na wengine 18 kujeruhiwa mkoani Morogoro.

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 11:40 jioni ilipata ajali hiyo baada ya utelezi uliosababishwa na kunyesha kwa mvua wakati mashabiki hao wakisafiri kwenda Shinyanga kusipa sapoti klabu yao katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Simba SC na Kagera Sugar utaochezwa kesho kwenye uwanja wa Kambarage.

Maiti ya ajali hizo wamehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro sambamba na majeruhi hao 18 kupatiwa huduma ya kwanza.

Mwenyezi mungu awalaze roho za marehemu mahala pema peponi na kuwapa unafuu majeruhi wote katika ajali hiyo.
AMINA

SOURCE:JUMA MTANDA BLOG
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger