Tuesday 21 April 2015

MAJAMBAZI WAUWA WAWILI NA KUPORA PESA ZA KAMPUNI YA BONITE MOSHI

...
Mlinzi wa Kampuni ya Bonite, aliyetambulika kwa jina la Shamba baada ya kupigwa risasi na majambazi mjini Moshi.
Dereva wa Kampuni ya Bonite aliyetambulika kwa jina moja la Mselemu mara baada ya kushambuliwa kwa risasi na majambazi.
...wakiwa kwenye gari baada ya kushambuliwa kwa risasi na majambazi.
Mlinzi baada ya kuuawa na majambazi.
MAJAMBAZI yaliyokuwa na silaha yamevamia gari mali ya Kampuni ya Bonite na kuwamiminia risasi dereva wa gari hilo aliyetambulika kwa jina moja la Mselemu na mlinzi wa Kampuni hiyo aliyetambulika kwa jina la Shamba kisha kupora fedha na kutokomea kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea jana mjini Moshi ambapo majambazi wanne waliokuwa kwenye pikipiki walivamia gari la Bonite lililokuwa likitoka kuchukua pesa za mauzo ya kampuni hiyo.
Taarifa zinadai kuwa dereva na mlinzi wa gari lililoshambuliwa walifariki palepale kutokana na kupigwa risasi nyingi sehemu mbalimbali za miili yao.
SOURCE:bongonewstz.com
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger