Thursday 30 April 2015

JESHI LA NIGERIA LAOKOA MATEKA WENGINE 160 KUTOKA MIKONONI MWA BOKO HARAM

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Jeshi la Nigeria wakiwa katika msitu wa Sambisa.

...wakiwa katika magari ya jeshi kuelekea kwenye mapigano.
JESHI la Nigeria leo limewaokoa mateka wengine 160 waliokuwa wanashikiliwa na wapiganaji wa Kiislam wa Boko Haram katika msitu wa Sambisa ambapo kwa sasa wanahesabiwa kuhakikisha idadi yao.
Hii imetokea ikiwa ni oparesheni endelevu ya kulisambalatisha kundi la Boko Haram nchini humo, baada ya Jeshi hilo kuivamia ngome ya Boko Haram iliyopo katikati mwa msitu wa Sambisa ampapo juzi wanawake 93 na wasichana 200 waliokolewa na Jeshi la Nigeria kutoka mikononi mwa wapiganji wa Boko Haram
"Bado tunawahesabu kupata idadi sahihi, lakini tayari kuna wanawake 60  wa umri mbalimbali na watoto wapatao 100,” alisema Kanali Sani Usman akizungumza na shirika la habari la AFP, akaongeza kwamba tayari wamepelekwa katika eneo salama.
Hata hivyo, katika oparesheni ya kuwapata, mwanamke mmoja aliuawa na wanane miongoni mwa mateka walijeruhiwa.
Vilevile, Aprili 28, jeshi la Nigeria liliwaokoa wanawake na wasichana 293 kutoka msitu huo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger