Sunday 26 April 2015

BREAKING NEWS:"MVUA YASABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI TANGA

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Watoto wawili wamekufa huku wengine wawili wakijeruhiwa vibaya baada ya ukuta wa nyumba waliyokuwa wamelala kuwaangukia na kuwafunika kitandani kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha mkoani Tanga.

Wakizungumza na Mpekuzi katika eneo la tukio lililopo barabara ya 18 jijijni Tanga viongozi wa serikali na wale wa wananchi wa eneo hilo wamesema limetokea jana majira ya saa 11 Alfajiri wakati mvua iliyoambatana na upepo ikinyesha ndipo ukuta wa nyumba hiyo uliojengwa na mawe makubwa ya baharini ulipodondoka na kusababisha madhara hayo.
 
Waliokufa katika eneo hilo wametajwa kuwa ni Bakari Shabani mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Ngamiani kati na Hassan Abdala mwenye umri wa mwaka mmoja ambao walifariki papo hapo huku wengine wawili wakijeruhiwa vibaya akiwemo mama mzazi wa marehemu ambao wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo.
 
Kufuatia hatua hiyo diwani Mbaruk ameiomba halmashauri ya jijij la Tanga pamoja na idara ya majengo kufanya ukaguzi wa majengo chakavu hasa katika kipindi hiki cha mvua za masika ili baadhi ya familia ziweze kuhamishwa na kutafutiwa mahali pa kujisitiri ili kuepuka maafa makubwa dhidi ya wahusika
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger