Saturday 25 April 2015

NEWS:WATU 560 WAFARIKI KWA TETEMEKO LA ARDHI NCHINI NEPAL

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Majengo yaliyoporomoshwa kwa tetemeko la ardhi nchini Nepal.

Majeruhi baada ya kuokolewa wakati wa tetemeko hilo.

Tetemeko kubwa la ardhi limekumba eneo lililo Magharibi mwa Nepal karibu na Mji Mkuu wa Kathmandu .Maafisa wa polisi wamethibitisha kuwa zaidi ya watu 560 wamefariki dunia huku wengi wakiwa hawajulikani waliko na kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka.
Shirika la utafiti la Marekani limesema kuwa tetemeko hilo la vipimo vya 7.9 lilikumba eneo lililo umbali wa kilomita nane Mashariki mwa Pokhara Magharibi mwa mji Mkuu wa Kathmandu.
Kuna ripoti za uharibifu wa majengo na bidhaa, makazi ya watu hata miundo mbinu ya Mawasiliano ya simu nayo yameharibiwa vibaya.
Picha za majengo yaliyokuwa yameporomoka pamoja na mahekalu ya miaka mingi iliyopita zimeonekana kwenye mitandao ya kijamii.
Walioshuhudia walisema kuwa watu walikimbia nje ya majengo muda mfupi baada ya tetemeko hilo kutokea.
Mitetemeko mingine midogo imesikika kaskazini mwa India pamoja na nchini Pakistan. (BBC)

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger