Monday 27 April 2015

NEWS:"PIUS MSEKWA ASIMULIA MAWIMBI YA MUUNGANO,TANZANIA"

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Maggid Mjengwa's photo.
Ndugu zangu,
Nchi yetu ina watu wachache aina ya Pius Msekwa

ambao hatuwatumii vema kwenye kutoa maarifa yao kwa umma kutokana na uzoefu wao. Redio na Runinga zingetumika vema kuchota maarifa hayo kupitia mahojiano makini.
Chini ya nusu saa Pius Msekwa ameweza kuelezea mambo ya msingi kuhusu Muungano kama alivyoyashuhudia mwenyewe akiwa mtendaji kijana ikiwamo kuwa Katibu wa Bunge.
Pius Msekwa anapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa wanasiasa na watendaji wengine. Kwamba wajenge mazoea ya kuandika vitabu.
Kwenye maktaba yangu nina vitabu hivyo viwili vya Pius Msekwa. Na hakika, kama mzazi, ukivisoma na kuvielewa, unaweza kuwa mwalimu mzuri kwenye kumsaidia mtoto wako kuelewa historia ya kisiasa ya nchi hii baada ya uhuru. Mathalan, Msekwa anachambua kwa kina chimbuko la Muungano kwenyw Uongozi Na Utawala wa Mwalimu Julius Nyerere. ( Ukurasa wa 83-88)

Maggid Mjengwa's photo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger