Aidha Rais Kikwete aliagiza viongozi wa mapango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kuliingiza suala la afya katika mpango huo.
Changamoto
hiyo imetolewa leo na Rais Kikwete kabla ya kuzindua mpango huo,
ulioenda sambamba na uzinduzi wa kadi ya ufuatiliaji(scorecard) ambayo
itakuwa inaonesha tathimini na ya maendeleo na mkakati huo kwa kila
mkoa na wilaya.
Rais
Kikwete aliwataka wakuu hao na watendaji wao kutoa ripoti ya kadi ya
ufuatiliaji kila baada ya miezi minne. Kadi hiyo, ambayo itakuwa na
taarifa ya maendeleao ya kupunguza vifo vya watoto wachanga, chini ya
miaka mitano na wakinawajawazito.
Uzinduzi huo, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam.
Alisema
vifo vya uzazi vya wakina mama vimepungua kutoka 578 kwa vizazi hai
100,000 mwaka 2005 na kufikia vifo 454 kwa vizazi hai 100,000 kwa sasa,
wakati lengo la milenia ni vifo 193 kwa vizazi hai 100,000.
“ Bado
tuna safari ndefu ninawataka wakuu wa mikoa na wilaya kuchulikia jambo
hili kwa umakini na kulipa kipaumbele kwani jukumu hili si la waganga
wakuu wa mikoa au wilaya na mimi nitakuwa ninafuatilia kwa kuwa jambo
hili, lipo mikononi mwangu. Ninataka kulifuatialia kabla sijamaliza
kipindi cha uongozi wangu,” alisema Rais Kikwete.
Aliongeza
kuwa vifo hivyo vya wakina mama na watoto hutokea lakini havifatiliwi
ndio maana inakuwa vigumu kubaini njia za kuvipunguza.
“Baya
zaidi wanakufa kwa sababu zinazoweza kuzuilika, kadi ya ufuatiliaji
ikifuatiliwa na wakuu wa mikoa itasaidia kupunguza vifo,” alisisitiza.
Alisema
ikiwa watoto waliochini ya miaka mitano na wakinamama wajawazito
watazingatia masuala ya lishe bora kwa kipindi cha siku 1000 pia
itasaidia kupunguza vifo hivyo.Huku akisema vyakula hivyo vipo majumbani
kinachohitajika ni elimu.
Aliwataka
wakimama kuzingatia uzazi wa mpango(nyota ya kijani ) ili kusaidia
kupunguza tatizo hilo, pia kushirikisha wanaume juu ya jambo hilo.
Rais
Kikwete pia alisema asilimia 51 ya wakina wanaojifungua huhudumiwa na
watalaamu wenye ujuzi, wakati malengo ya milinea ni asilimia 80, hivyo
bado kuna changamoto ya asilimia 29.
Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe, alisema kwa kipindi cha mwaka huu wanampango wa kuajiri watalaamu hao 11,021.
Alisema
Tanzania imefanikiwa kutimiza lengo la milinea namba nne kabla ya wakati
kwa kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kwa kiwango cha 54
kwa watoto wanaozaliwa 1000, kutoka 165 kwa wataoto wanaozaliwa 1000
mwaka 1990. Alizitaja nchi nyingine zilizofanikiwa ni Rwanda,
Malawi,Ethiopia Rwanda na Malawi.
Naye
mwakilishi wa wakuu hao, Dk. Christine Ishengoma alisema uwajibikaji wa
viongozi na watendaji ni jambo la muhimu katika kutekeleza mpango huo,
hivyo suala hilo linawezekana.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI), Dk. Deo Mutasiwa alisema sheria ndogondogo
zinatengenezwa ili kuwezesha mpango huo kufikia lengo.
Dk.
Mutasiwa alizitaka halimashauri kutumia vyanzo vyake vya mapato ya ndani
kwa asilimia 60 kuwekeza katika masuala ya afya, elimu maji na barabara
za vijijini.
Alisema
hivi sasa wako katika mchakato wa kupata kibali cha kuwaezesha watoa
huduma wa afya wanaomba nafasi za kazi kufanyia kazi maeneo wanayotoka.