Tuesday, 3 December 2024

TBS YATOA ELIMU KUHUSU VIWANGO NA UBORA WA BIDHAA MKOANI SONGWE

...

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa Elimu kwa umma kuhusu masuala ya Viwango katika ngazi za wilaya ambao elimu hiyo imetolewa katika Halmashauri za wilaya za Mbozi, Songwe, Momba na Halimashauri ya Tunduma mji mkoani Songwe.

Akizungumza wakati wa Kampeni hiyo, Afisa Masoko TBS Bw. Mussa Luhombero amesema lengo la Shirika hilo ni kutoa Elimu Kwa Umma kuhusu umuhimu wa kusoma taarifa zilizopo katika bidhaa, kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake sambamba na kuwahamasisha wajasiriamali wadogo kuthibitisha ubora wa bidhaa zao na wafanyabiashara kusajili maduka ya chakula na vipodozi.

Kampeni hiyo ya Elimu kwa umma imefanyika katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Sokoni, Stendi, Minadani na maeneo mengine ya wazi ambapo wananchi walijitokeza kupata elimu na ufahamu wa masuala mbalimbali yahusuyo Ubora wa Bidhaa.

Luhombero amewasisitiza wajasiriamali na wafanyabishara kuhakikisha wanauza bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS na wenye majengo ya bidhaa za chakula na vipodozi kuyasajili ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

Aliongeza kwa kuwafafanulia wananchi umuhimu wa viwango katika maisha yao ya kila siku na kuwaasa wawe mabalozi wa kuhamasisha ubora katika jamii wanazoishi sambamba na kutoa taarifa katika ofisi ya TBS zilizopo karibu au kupiga katika kituo cha huduma kupitia mawasiliano yaliyotolewa iwapo watakutana na changamoto zihusuyo masuala ya ubora wa bidhaa wakati wa manunuzi.

Wananchi wamelipongeza Shirika la Viwango Tanzania Kwa kutoa Elimu hiyo kwani itawasaidia kufanya maamuzi sahihi wakati wa kununua bidhaa.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger