Kampeni ya Selebretika Kijamukaya 'Sisi Ndio Sikukuu Yenyewe' inayoendeshwa na Kampuni ya Jambo Group Msimu huu wa Sikukuu imezinduliwa rasmi na sasa imefika katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga.
Katika hatua hiyo, akina mama wajawazito na waliojifungua wamefikiwa na kufurahia bidhaa maalumu za Jambo, ikiwa ni pamoja na biskuti na vinywaji vyenye chapa au logo maalum ya Jambo Msimu wa Sikukuu, vyote vikiwa na ladha ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2025.
Kampeni hii ilizinduliwa rasmi Desemba 21, 2024, kwenye Ofisi za Jambo Media zilizopo Ibadakuli Mjini Shinyanga.
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa wa Kampuni ya Jambo Group, Nickson George, amesema kampeni hiyo ni sehemu ya juhudi za kuwafikia wateja na watumiaji wa bidhaa za kampuni hiyo, ili waweze kufurahia bidhaa za Jambo na familia zao wakati wa msimu wa sikukuu.
“Lengo letu ni kuleta furaha na ladha ya Jamukaya kwa familia nyumbani, hivyo tumekuja na vinywaji maalumu vyenye logo maalum ili kufanya sikukuu iwe tamu zaidi. Vinywaji vyetu pia ni vya manufaa kwa afya, kwa sababu vina sukari rafiki kwa wale wanaochangia damu,” amesema George.
Ameongeza kuwa ili familia iweze kufurahia sikukuu ipasavyo, bidhaa za Jambo zinapaswa kuwa sehemu ya meza ya chakula kila siku: Asubuhi ukiamka, vitafunwa vya Jambo, maji ya Jambo, juisi za Jambo, biskuti za Jambo, Ice Cream za Jambo - bidhaa hizi zitafanya sikukuu iwe yenye ladha ya kipekee.
Kampeni ya Selebretika Kijamukaya inaendelea kuhamasisha watu kufurahia bidhaa za Jambo wakati wa msimu wa sikukuu na kuhakikisha kuwa nyumbani kunakuwa na ladha ya Jambo muda wote.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kambarage, Ernest Magula, pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Kituo hicho, Adolf Nsanzungwanko, wameishukuru Kampuni ya Jambo Group kwa kutoa zawadi za Sikukuu kwa wagonjwa, wakiwemo akina mama wajawazito na waliojifungua katika msimu huu wa Krismasi na Mwaka Mpya.
Magula na Nsanzungwanko wameeleza kuwa zawadi hizo zimeleta faraja kwa wagonjwa, huku wakisisitiza umuhimu wa ushirikiano na wadau wengine ili kuendelea kusaidia katika kuboresha huduma za afya.
Wamesema changamoto zinazokikabili kituo hicho ni pamoja na upungufu wa damu salama na ukosefu wa uzio wa kuimarisha usalama.
Kwa upande wao, akina mama waliokutwa katika wodi ya wazazi, akiwemo Fortunatha Athanas na Juliana Shija, wameishukuru Kampuni ya Jambo Group kwa kutoa zawadi hizo za Sikukuu, huku wakiipongeza kwa ubunifu wake.
Wamesisitiza kuwa watendelea kutumia bidhaa za Jambo hata majumbani mwao kwa sababu wanaziamini na kuzithamini.
0 comments:
Post a Comment