Sunday, 1 December 2024

SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE

...
 
Utendaji kazi wa kiwango cha juu wa Rais Samia Suluhu Hassan, umewezesha eneo kubwa la nchi kuwa na uhakika wa kupata maji safi na salama kwa mijini na vijijini hali iliyoifanya Serikali kutaka mafanikio hayo yalindwe.

Ikumbukwe kuwa  hadi kufikia Februari 2024, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika maeneo ya vijijini ilifikia asilimia 79.6 ikilinganishwa na asilimia 77 Februari, 2023.

Kwa upande wa mijini upatikanaji wa maji umefikia asilimia 90 ikilinganishwa na asilimia 88 Februari 2023.

Mafanikio hayo ni makubwa na ndio yamempa nguvu Kaibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuwataka watumishi wa Sekta ya Maji kuhakikisha wanalinda mafanikio yaliyofikiwa katika utekelezaji wa majukumu ya sekta hiyo.

Mhandisi Mwajuma ametoa agizo hilo katika kikao chake na watumishi wa Wizara hiyo jijini  Dodoma.

Ikumbukwe kuwa Serikali ya Rais Samia, kupitia Wizara ya Maji, imeweka malengo makubwa ya kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa uhakika wa maji safi na salama kwa wananchi wote nchini. 

Malengo haya ni sehemu ya juhudi za kufikia Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Kwa mujibu wa mpango wa serikali ni kuhakikisha huduma ya maji safi na salama inawafikiwa asilimia 95% ya wakazi wa mijini ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wa wananchi wa Vijijini asilimia 85 wawe wanapata huduma ya maji safi na salama ifikapo mwaka 2025.

Malengo hayo yanategemewa kufanikishwa na miradi mbalimbali kama Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP), ambayo inalenga kuboresha miundombinu ya maji na kuongeza upatikanaji wa maji vijijini na mijini. 

Serikali pia inashirikiana na sekta binafsi na mashirika ya kimataifa ili kufanikisha malengo haya.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger