Wednesday 12 May 2021

Zaidi ya wagonjwa Mil. 20 Watibiwa 2020/21- Serikali

...

 


Na Nteghenjwa Hosseah, Manyara
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, anayeshughulikia Afya, Dkt. Grace Maghembe amesema katika mwaka wa fedha 2020/21 wauguzi waliopo katika vituo vya kutolea huduma wamehudumia wagonjwa wapatao milioni 20 waliofika katika vituo hivyo kupata huduma za kiafya.

Akitoa salamu za Ofisi ya Rais TAMISEMI wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Manyara. Dkt. Magembe ameyasema, huduma zilizotolewa kwa wingi ni pamoja na huduma za Nje maarufu kama huduma za Mkoba  ambazo zilihusiaha takribani watu milioni 1.2 ambazo zimejikita zaidi katika kumhudumia mama na mtoto.

Dkt. Magembe, amesema wauguzi hao walifanikiwa kuwazalisha kina mama takribani laki moja na kutoa huduma dawa ya usingizi kwa wajawazito 25,000.

Dkt. Magembe, alibainisha mahitaji ya wauguzi wa sasa ni 41,000 lakini waliopo katika vituo vya kutolea huduma ni 19,000 ambapo ni sawa na asilimia 41 ya mahitaji.

Kuhusiana na wauguzi walio ajiriwa katika mwaka wafedha wa 2017/2019  ni 3,625 ambapo watumishi hao waliajiriwa na Serikali pamoja na wadau  wa Taasisi ya Benjamini Mkapa.

"Na katika ya ajira 2,720 za kada ya afya zilizotangazwa Mei 9 mwaka huu na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, jumla ya ajira za wauguzi miongoni mwake ni 954 sawa na asilimia 35 ya ajira zote zilizotangazwa."

Siku ya wauguzi husherehekewa tarehe 12 mwezi Mei ya kila Mwaka, ambayo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Florence Nightngale, mwana takwimu na mwanzilishi wa uuguzi wa kisasa. Maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani kitaifa yamefanyika mkoani Manyara na kubebwa na kauli mbiu “Wauguzi sauti inayoongoza, Dira ya huduma ya afya”


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger