Thursday, 20 May 2021

WAZIRI MKUU ATAKA HATUA ZAIDI ZICHUKULIWE WALIOZINGUA MFUMO WA LUKU.... "WAKAE PEMBENI..UCHUNGUZI UFANYIKE"

...


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amemuagiza Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani asiishie kuwasimamisha kwa siku kumi tu meneja wa TEHAMA na wasaidizi wake, bali wakae pembeni hadi hapo uchunguzi zaidi utakapokamilika.

Ametoa agizo hilo leo Mei 20, 2021 alipozungumza na Menejementi na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwenye makao makuu ya zamani Shirika hilo jijini Dar es Salaam.

“Lazima tufundishane kuwa makini, kila siku lazima tukague vifaa vyetu ili huduma ipatikane muda wote. Hakuna kuwasimamisha kwa siku 10, wakae pembeni hadi timu inayochunguza itakapotoa matokeo.  Inawezekana sio wao tu, Waziri endelea na uchunguzi”

Aidha, Waziri Mkuu ameliagiza shirika hilo kuhakikisha wanakuwa na mfumo wa dharura ‘backup’ utakaotumika pindi kunapotokea changamoto za kimfumo

“Mmetengeneza usumbufu mkubwa sana, mlijua lazima kuwe na backup lakini hakuna, toka pale tulipoanza kutoa huduma mpaka leo kwanini hakuna backup, hilo ni jukumu lenu”

Amesema kuwa Serikali inataka kuona huduma hii inapatikana muda wote. “Jitihada za Serikali kuimarisha vyanzo vya umeme zina lengo la kuhakikisha tunapata umeme mwingi na wa gharama nafuu".

Naye, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema hakuridhishwa na watendaji wanaosimamia mfumo na amewaomba radhi watanzania kwa usumbufu uliojitokeza.

Pia amesema amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Nishati aunde kikosi kazi maalum kwa ajili kuupitia upya mfumo

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger