Friday, 7 May 2021

WAFANYAKAZI WA HOSPITALI WAKAMATWA KWA WIZI WA NETI ZA MBU HOSPITALI

...
Maafisa wa polisi katika kaunti ya Kisumu nchini Kenya wamewakamata wafanyakazi watatu wa hospitali kwa kuhusika na wizi wa neti za mbu 17,050. 

Theresa Anyango Otieno, kaimu afisa katika hospitali eneo la Rabuor; Cynthia Akinyi, kaimu afisa anayeshughulikia usambazaji wa neti katika eneo la Nyang’ande; na David Ouma, afisa anayesimamia hospitali ya Nyang'ande wote walikamatwa Ijumaa, Mei 7,2021. 

Kulingana na kamanda wa polisi wa kaunti ya Kisumu, Samuel Anampiu, watatu hao walihusishwa na kutoweka kwa mabunda 181 yaliyokuwa katika hospitali ya Nyang'ande na mabunda mengine 160 kutoka hospitali ya Rabuor, kila bunda likiwa na neti 50. 

"Tumewakamata wafanyakazi watatu wa hospitali ambao tunaamini walihusika na wizi wa neti tangu walipoanza kusimamia usambazaji, " Anampiu alisema.

 Kamanda wa polisi aliongeza kuwa bado wanawatafuta washukiwa wengine wawili, ambao ni Dickson Malit, aliyekuwa akihudumu katika hospitali ya kaunti ndogo ya Rabuor na vile vila Samuel Omino. 

Kukamatwa kwao kulijiri kufuatia malalamiko kutoka kwa wenyeji ambao walikuwa wamejitokeza kwa ajili ya kupokea neti za bure lakini wakarudishwa nyumbani baada ya kuarifiwa kuwa zimeisha. 

Kwa kawaida neti husambazwa na serikali bila malipo kwa familia ambazo zinaishi katika maeneo ambayo huvamiwa na mbu.

Chanzo - Tuko News



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger