Tuesday 11 May 2021

TCRA YAWATAKA WATUMIAJI WA MITANDAO YA KIJAMII KUWEKA 'PASSWORD'

...

Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji TCRA, Dkt. Philip Filikunjombe

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka Watumiaji wa Mitandao ya Kijamii wakiwemo Waandishi wa Habari Mtandaoni kuweka Nywila 'Passwords' ili kuzuia matumizi ya mitandao au vifaa vya mawasiliano bila idhini ya mhusika.


Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji TCRA, Dkt. Philip Filikunjombe leo Jumanne Mei 11,2021 mkoani Morogoro wakati wa semina kwa Waandishi wa Habari Mtandaoni (Online Media Journalists, Bloggers and Editors) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

Dkt. Filikunjombe amesema ni lazima kila mtumiaji wa kifaa cha mawasiliano ikiwemo Simu ya Mkononi na Computer aweke Password ili kulinda taarifa zake ikiwa ni pamoja na kuepuka watu wasio wema kutumia vibaya mtandao.

"Pia tunapaswa kulinda watoto mtandaoni 
kwa kutowapa simu zetu. Usimpe simu yako mtoto kwa sababu kuna mambo mengine hayapaswi kuonwa na watoto kwa umri wao. Jitahidi kuweka Neno la Siri (Password) kwenye simu yao", amesema Dkt. Philikunjombe.

Katika hatua nyingine amewataka waandishi wa habari mtandaoni kuepuka kusambaza taarifa za uongo 'Fake News' na kutumia lugha mbaya huku akiwasisitiza kusajili vyombo vya habari mtandaoni ili kuepuka kujiingiza katika migororo ya kisheria.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger