Samirah Yusuph.
Bunda. Katibu tawala wa Wilaya ya Bunda Halfan Mtetela ametoa wito kwa wakala wa barabara mjini na vijijini TARURA kufanya marekebisho ya mara kwa mara barabara za ndani ya hifadhi ili kurahisisha shughuli ya utalii.
Wito huo umeutoa jana wakati wananchi wa wilaya ya Bunda walipotembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti upande wa Kilawira na kusisitiza kuwa kila mtu ahamasike kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo mbuga za wanyama na hifadhi za taifa.
“Barabara zikiwa hazijatengenezwa vizuri inakuwa changamoto kupitika ni lazima wakala wa barabara vijijini na mjini (TARURA) kuona umuhimu wa kizitengeneza na ikiwezekana kuongeza bajeti ili kusaidia kwenye matengenezo hayo, zitasaidia kuvutia watalii na kufika eneo husika kwa urahisi na kwa wakati,”amesema Mtekela.
Alisema Watanzania wanapaswa kuwa wazalendo kwa kupenda vivutio vyao na kuvitangaza ili kufanya idadi ya watanzania wanaotembelea hifadhi na mbinga za taifa iongezeke.
"Kila mmoja anapaswa kuwa balozi wa kutangaza vivutio kwenye mtandano kupokea watalii kutoka ndani na nje kwani kufanya hivyo kutapelekea kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya NCT twende kutalii Albart Chenza alisema katika kuhakikisha watanzania wengi wanatembelea hifadhina vivutio hivyo,kampuni yake kwa kushirikiana na uongozi wa Serengeti wameanzisha mpango wa kutembelea taasisi na wananchi ili kuhamasisha wananchi hao wanatembelea hifadhi hizo
“Hifadhi ya Serengeti imeanzisha mpango unaoitwa mlango kwa mlango…na sisi kampuni yetu tunaunga mkono na kuhamasisha wananchi na mpaka sasa mwamko umeanza kuonekana.
Nae Gilango Nyarunge mfugaji wa kijiji cha Salangwe Bunda ambaye amepata fursa ya kutembelea hifadhi ya Serengeti alisema amejifunza vitu vingi na kuahidi kuhamasisha wenzake kuwa na desturi ya kutembelea hifadhi hizo.
"Watanzania tupo zaidi ya milioni 60 kwa sasa lakini ukiangalia idadi ya watu wanaoingia kwenye hifadhi zetu kuangalia utalii ni wachache kuliko idadi ya watu waliopo nchini hali hii inaonyesha sisi siyo wazalendo ni vyema tupende utalii wa kwetu wa ndani .
mwisho
0 comments:
Post a Comment