MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Judica Omari |
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi msaada huo wa pili kutoka kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Judica Omari |
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella ametoa msaada wa chakula na vifaa mbalimbali kwa makundi ya watu wenye mahitaji maalumu mkoani humo vyenye thamani ya Sh .Milioni 3.6 kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Fitri.
Msaada huo umekabidhiwa kwenye makundi hayo maalumu ya watu wenye mahitaji maalumu kupitia kituo cha Wazee cha Mwanzange,Misufini na kituo cha Kulea Watoto wenye mahitaji maalumu kilichopo eneo la Pongwe Jijini Tanga katika halfa iliyofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Msaada uliotolewa ni pamoja na Mbuzi wa tano,mchele,mafuta ya kula,sabuni,mashuka,mavazi na vyengine kwa ajili ya huduma za afya ikiwemo Taulo za kike na pampasi.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo,RC Shigella alisema kwamba wameamua kutoa msaada huo ili kuwawezesha makundi hayo maalumu waweze kusheherekea sikuuu ya Eid El Fitri vema kwa kuwawezesha mahitaji hayo muhimu
Alisema wameona waweke utaratibu huo mzuri zaidi badala ya kuwaalika na kula nao pamoja wakaona waandae kutengeneza chakula kwa ajili ya sikukuu wakiwa kwenye maeneo hayo kwa kusheherekea.
“Nimpongeze Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari na Menejimenti ya Ofisi kwa utaratibu huu ambao unaenda kugusa furaha ya ndugu zetu waliopo kwenye mazingira magumu na mazingira ya uhitaji na msaada huu ni mahususi kwa ajili ya Sherehe kwani kipindi cha siku 30 waislamu kote dunia na mkoa wa Tanga wameshiriki kikamilifu kwenye kufunga na kwenye funga ndio mahala pekee walikuwa wakiwasiliana na mwenyezi mungu kwa ajili ya toba na kuiombea nchi yetu”Alisema
Mkuu huyo wa Mkoa alisema wanapohitimisha funga wanakuwa na sherehe watu wanasherekea na kuomba baraka wakaona watengeneza utaratibu wa kugusa nafsi na nyoyo za makundi hayo maalumu mkoani Tanga ili angaliu watakaposherehe wasihangaike wapata wapi chakula kwani angalau vitu hivyo vikiwepo wanaweza kusheherekea vizuri.
“Nitumie nafasi hii kuwapongeza viongozi wa dini kwa namna walivyoshiriki kwenye kipindi cha mwenzi wa ramadhani watu wameendelea kushirikiana hivyo tuendelee kuiweka nchi yetu kwenye maombo ili Rais wetu Samia Suluhu aweze kuyatumiza malengo aliyokusudia kwenye kipindi chake cha awamu ya sita”Alisema RC Shigella.
Hata hivyo aliwatakia waislamu kote nchini na mkoani Tanga maadhimisho mema ya sikukuu ya Eid El Fitri huku akieleza kwamba wataimarisha ulinzi na usalama ili wananchi mahala watakaposhiriki washeherekee kwa usalama,amani na furaha.
Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari alisema mkuu wa mkoa ametoa mchango wake kwenye mwezi huu wa ramadhani kwani ameona kama mkoa wasiweze kuishia kimyakimya wao waweze kushiriki kutoa sadaka kwa dugu zao wazee wanaoishi kwenye vituo vya serikali na watoto wanaoisni kwenye mazingira magumu.
Hata hivyo aliwatakia heri ya sikuuu ya Eid El Fitri waislamu wote mkoani Tanga na kuwataka washeherekee kwa utulivu na amani
Naye kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Tanga Imani Clemence alisema vituo ambavyo vimeainishwa kupatiwa mahitaji hayo ni kituo cha Wazee Mwanzange,Kituo cha Wazee Misufini na Kituo cha watoto wenye mahitaji Maalumu cha Pongwe .
Imani alisema mafanikio walioyapata ni Serikali kutenga fedha kwa ajili ya kutatua changamoto nyingi zilizokuwa zinakabili makazi ya wazee mfano huduma ya afya ambapo kwa sasa imetenga fedha kwa ajili ya kununua dawa ambazo hazipatikani hospitalini.
“Lakini mafanikio mengine ni Serikali kutenga fedha kwa ajili ya matumizi madogo ya vituo kama dharura ndogo ndogo zinazojitokeza”Alisema
0 comments:
Post a Comment