Akizungumza wakati wa kukabidhi ripoti hiyo, mwenyekiti wa Kamati hiyo, Prof. Said Aboud amesema;
“Tangu kuingia kwa Covid 19 Tanzania March 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika Mataifa mengine Duniani, kuna tishio la kutokea wimbi la tatu nchini.
“Chanzo ya COVID-19 itolewe kwa vipaumbele kwa kuanzia kwa wahudumu wa afya, watumishi wa umma, viongozi wa dini na mahujaji, wazee, wenye maradhi sugu, watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama na wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.
“Kamati inaishauri serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na WHO ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake.
“Kamati imebaini kuwa mwamko wa kudhibiti wimbi la kwanza la Corona ulikuwa mkubwa ukilinganisha na wimbi la pili, Kamati imeshauri kuimarisha kasi kudhibiti tishio la wimbi la tatu.
“Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa Covid 19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za kinga katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.
“Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya Kikanda na Kimataifa iliyoridhia katika Jumuiya za Afrika Mashariki, SADC, AU na WHO,” amesema Prof. Said Aboud.
0 comments:
Post a Comment