Waziri wa Viwanda na Biashara na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa EPZA, Prof. Kitila Mkumbo ameongoza kikao cha kawaida cha 32 cha bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya nje (Export Processing Zones Authorty -EPZA).
Kikao kimefanyika Mei 19, 2021 Jijini Dodoma katika ukumbi wa Mkutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Jengo la Mkapa na kimeudhuliwa na viongozi mbalimbali; Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dotto James, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Mathew Mnali na wajumbe wengine wa bodi ya wakurugenzi wa EPZA.
Kikao hicho kimekuwa na lengo la kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkurugenzi wa EPZA kwa kipindi cha Januari – Machi 2021, Makadirio ya mapato na matumizi ya Mamlaka ya (EPZA) kwa mwaka 2021/2022, utaratibu wa kuendeleza Mradi wa kurasini SEZ, mradi wa kubangua korosho kwa kushirikiana na wajasiriamali (SMEs) na mengineyo
0 comments:
Post a Comment