Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Joseph Malongo,akifungua mafunzo ya Wahandisi yanayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Mei 19 hadi 21,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Joseph Malongo,akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo ya Wahandisi yanayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Mei 19 hadi 21,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Joseph Malongo,akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya Wahandisi yanayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Mei 19 hadi 21,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Wahandisi wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Joseph Malongo,(hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya Wahandisi yanayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Mei 19 hadi 21,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi,Mhandisi Ninatubu Lema,akizungumza wakati wa mafunzo ya Wahandisi yanayofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma kuanzia leo Mei 19 hadi 21,2021.
Msajili wa Bodi ya Wahandisi,Mhandisi Patrick Barozi,akielezea lengo la mafunzo hayo ya Wahandisi yanayofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma kuanzia leo Mei 19 hadi 21,2021.
Msajili wa Bodi ya Wahandisi,Mhandisi Patrick Barozi,akionyesha kitabu chenye mwongozo wakati wa mafunzo ya Wahandisi yanayofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma kuanzia leo Mei 19 hadi 21,2021.
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Malongo,amefungua mafunzo ya siku tatu ya Wahandishi wenye lengo la kujadili miradi ya kimkakati ili iweze kusaidia Taifa katika utekelezaji na usimamizi wa miradi hiyo huku akiwataka kutembelea miradi mikubwa nchini ili kujionea changamoto zilizopo.
Akizungumza leo Mei 19,2021 wakati akifungua mafunzo hayo kuhusu uendeshaji wa maswala ya miradi ya kimkakati kwa wahandisi itakayosaidia kukidhi mahitaji ya watanzania yalioandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini (ERB) yanayofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.
Mhandisi Malongo amesema kuwa Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye sekta ya ujenzi hivyo wahandisi wanatakiwa kupata elimu ili kukabiliana na malalamiko kwa Wahandisi kwenye utekelezaji wa miardi yao.
Amewataka kuanzisha mafunzo yajayo yasihusishe wahandisi pekee bali ihusishe wote wanaofanya miradi kutimia.
“Ni vizuri tukianzisha mafunzo mengine tuhakikishe kuwa wahandisi, watunza fedha na wanasiasa watakuwepo ili kuwe na mchanganuo mzuri wa mawazo” amesema Mhandisi Malongo
Hata hivyo ameipoongeza bodi ya usajili wa wahandisi (ERB) kwa kuanzisha mafunzo hayo badala ya kuitegemea serikali kujiendeleza kitaaluma kwani ilikuwa inawarudisha nyuma wahandisi.
Aidha amewaomba wahandisi kuanza kutembelea miradi mikubwa inayoendelea nchini ili kujifunza changamoto zilizopo na kuzipatia ufumbuzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi Ninatubu Lema amesema kuwa mafunzo hayo yatawajengea uwezo wahandisi kuhusu nini kifanyike katika kuendana na kasi ya teknolojia huku kuwaongezea elimu kuibua, kusimamia miradi ya kimkakati itakayoleta tija kwa Taifa.
Awali Msajili wa Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi, amesema kuwa mafunzo ya usimamizi wa miradi yataendelea kutolewa ili kuimarisha uwezo wa wahandisi nchini na kuwataka wahandisi wenye sifa kujisajili na Bodi hiyo.
0 comments:
Post a Comment