Friday, 21 May 2021

MBUNGE NEEMA LUGANGIRA AITAKA SERIKALI KUANZISHA MAHAKAMA YA FAMILIA “FAMILY COURT”

...
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akiuliza swali Bungeni Jijini Dodoma leo
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akiuliza swali Bungeni Jijini Dodoma leo
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira amesema ipo haja ya Serikali kuanzisha Mahakama ya Familia yaani Family Court kama ilivyofanya kwenye Mahakama za Ardhi ili kusaidia kuondosha changamoto zinazojitokeza ikiwemo Masuala ya Matunzo ya Watoto.

Amesema ili Matunzo ya Watoto yaweze kubebwa kwa uzito unaostahili na kupanua wigo mpana wa haki ili kuhakikisha changamoto za namna hiyo zinaondoka kwenye jamii badala ya kuendelea kuwepo kila wakati.

Aliyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati alipouliza Maswali Mawili ya Nyongeza baada ya Serikali kuwasilisha Majibu ua Swali lake la Msingi lililouliza "Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwakomboa Wanawake wanaobebeshwa mzigo mkubwa wa kugharamia matunzo ya Watoto bila msaada wa Baba?" 

Mbunge Neema alisema pamoja na majibu mazuri ya Serikali lakini hata kwa Sheria zilizopo bado kuna changamoto kubwa kwenye eneo hilo.

Mbunge Neema Lugangira alisema ndio maana hata Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye Ilani yake ya Uchaguzi 2020/2025 imeliona hilo na imeahidi kuielekeza Serikali kwenye Ukarasa wake wa 145 unaosema "CCM itaelekeza Serikali kuimarisha huduma za usuluhuhi wa migogoro ya ndoa na matunzo kwa watoto" na kwa msingi huo aliuliza maswali yake  mawili ya nyongeza.

Katika maswali yake ya nyongeza Mbunge Lugangira aliishauri Serikali iboreshe Sheria zilizopo ili gharama za matunzo ya watoto iendani na hali ya uchumi wa sasa na maisha ya sasa kutokana na maisha kuwa juu kuliko ilivyokuwa awali.

Akijibu Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Mhe Mwanaidi Khamisi amesema "Serikali imetoa maelekezo wazazi kuhakikisha mtoto anapata matunzo yote stahiki, na kama wazazi wa mtoto hawaishi pamoja na mtoto anaishi na Mama yake basi Baba atawajibika kugharamia malezi ya mtoto kulingana na kipato alichonacho". Swali hili pia lilimnyanyua Mhe Waziri Dkt Dorothy Gwajima ambae alisema "Nakiri tatizo Watoto kutelekezwa ni kubwa na ipo haja ya Serikali kufanya harakati za ziada ili kulidhibiti. 

Kwa upande mwingine Mbunge Neema Lugangira aliishauri Serikali ianzishe Mahakama ya Familia yaani Family Court na kwa upande wa Serikali, Mhe Naibu Waziri Mwanaidi Ali Khamis alisema Serikali imekubaliana na ushauri wa Mbunge Neema Lugangira na ipo haja ya kuwa na chombo maalumu ambacho kitakuwa kinashughulikia masuala la familia hivyo wameupokea ushauri wa Mbunge Lugangira na wataufanyia kazi  kulingana na Sheria zilizopo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger