Baadhi ya wanawake katika Kata ya Kashai Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, wamelalamikiwa kuwaoa wanafunzi wa kiume wa Shule za Sekondari Ihungo na Kahororo zote za Manispaa ya Bukoba Mkoani humo.
Katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na diwani wa kata hiyo Ramadhan Kambuga amesema kuwa suala hilo limekuwa kubwa na kuliomba jeshi la polisi kuanza msako wa kuwasaka wanafunzi hao na wake zao.
Amesema kuwa ni aibu mama mtu mzima kumuoa mtoto wa mwanamke mwenzake kwa kumlaghai na maneno yasiyo ya kawaida.
Akizungumza katika mkutano huo, mwakilishi wa mkuu wa shule ya Ihungo Mwl. Fraxon Msawile na wa Kahororo wamesema kuwa hali ya vijana ni mbaya na kuwaomba wananchi kuachana nao.
Wamesema kuwa vijana wengine hutoroka shule na kukimbilia kwa wanawake hao na wakati mwingine huvuta bangi..
0 comments:
Post a Comment