Thursday, 20 May 2021

INSPIRE TANGA YAIBUA MAAJABU YA UCHUMI WA KIDIGITALI KUPITIA UBUNIFU WA CHUPA YA CHAI KATIKA WIKI YA UBUNIFU

...
 Abdul Athumani akiwa na kifaa chake
Kijana Nzuri Bin Nzuri akiwa na kifaa chake

Ikiwa ni wiki ya ubunifu, Shirika la Masuala ya Sayansi la Inspire limeibua wabunifu mkoani Tanga ambao wakitumika vizuri wataleta Mapinduzi ya kisayansi ya uchumi wa kidigitali katika sekta ya viwanda na kilimo mkoani Tanga.

Fursa za wabunifu na ubunifu zimebainika katika ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya bidhaa za ubunifu yanayoendea katika viwanja vya kisosora jijini Tanga, ambapo kijana Nzuri Bin Nzuri wa Kijiji cha Gombero jijini Tanga ameibuka nyota katika tukio hilo kwa kuweza kubuni kifaa cha chupa ya chai chenye uwezo wa kuchaji simu, komputa, kusikiliza redio, kutazama Tv na kuwasha Taa.

Wakati Nzuri anafanya Mapinduzi ya sayansi ya digitali ya uchumi wa viwanda Abdul Athumani yeye amepata muarobaini kwa sekta ya kilimo na kuwa mkombozi wa wakulima kupitia kifaa chake chenye utambuzi wa kujua aina ya udongo, mimea inayostawi, mahitaji katika utunzaji wa mazao na upatikanaji wa masomo.

Meneja wa kituo cha Sayansi cha Kisosora jijini Tanga Gibson Kawago amesema lengo la maonesho hayo ni kuibua wabunifu, kuchochea vipaji vyao na kuvilea kwa nia ya kupata wataalamu, wanasayansi na wabunifu watakaojiinua kiuchumi katika mazingira wanayoishi kupitia ubunifu wao kwa maslahi mapana ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Akifungua maonesho hayo mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amehimiza kujiwekeza katika ubunifu wa kiuchumi wa kidigitali ili kwenda sambamba na mabadiliko ya kidunia ambayo yanaleta maendeleo endelevu kama ilivyo kwa simu za mikononi, huku akichagua Shirika la hilo kutembelewa na mbio za mwenge kwa namna linavyochangia kukua kwa vipaji na uchumi wa mkoa wa Tanga

Kauli mbiu ya wiki ya ubunifu ni "ubunifu kwa uchumi wa kidigitali stahimilivu na jumuishi" -  changia kukua kwa vipaji na uchumi wa mkoa huu .

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger