Monday, 17 May 2021

CCM WASHINDA UBUNGE JIMBO LA BUHIGWE NA MUHAMBWE

...

Mshindi wa uchaguzi mdogo wa ubunge, jimbo la Muhambwe kupitia CCM, Dkt. Florence Samizi.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Buhigwe, Bi. Marycelina Mbehoma (kulia), akimkabidhi Cheti cha ushindi mshindi wa kiti cha Ubunge Jimbo la Buhigwe, Felix Kavejuru.
***
Uchaguzi mdogo katika majimbo mawili ya Muhambwe na Buhigwe yote ya mkoani Kigoma, ambao ulifanya Mei 16, 2021 umemalizika kwa Chama Cha Mapinduzi kuibuka na ushindi katika majimbo yote.

Msimamizi wa uchaguzi wa ubunge Jimbo la Muhambwe, Bw. Diocles Rutema amemtangaza mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Florence Samizi kuwa mshindi wa kiti hicho kwa kupata kura 23,441.

Aliyefuatia ni mgombea wa ACT Wazalendo Bw. Masabo Julius aliyepata kura 10,847 na Mgombea wa Democratic Party (DP), Bw. Philipo Fumbo aliyepata kura 368.

Aidha msimamizi wa Uchaguzi wa ubunge Jimbo la Buhigwe, Bi. Marycelina Mbehoma amemtangaza Felix Kavejuru wa Chama Cha Mapinduzi, kuwa mshindi wa kiti hicho kwa kupata kura 25,274 kati ya kura 30320 halali zilizopigwa.


Felix Kavejuru amewashinda wapinzani wake 12 alioshiriki nao katika Uchaguzi mdogo uliofanyika Mei 16,2021.

Uchaguzi katika jimbo la Muhambwe umefanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM marehemu Atashasta Justus Nditiye aliyefariki mwezi Februari.

Kwa upande wa Jimbo la Buhigwe uchaguzi umefanyika baada ya aliyekuwa mbunge Dkt. Philip Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger