Mwakilishi kutoka Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Analyse Kaika akitoa elimu ya sheria mbalimbali za ulinzi wa mtoto na wanawake katika mafunzo kwa wanachama wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club- SPC).
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC), Patrick Mabula (aliyesimama) akitoa neno kwa wanachama wa klabu hiyo wakati wa mafunzo ya nafasi ya vyombo vya habari katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, John Tesha (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akifungua mafunzo ya nafasi ya vyombo vya habari katika kumaliza ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Na Damian Masyenene, Shinyanga
KATIKA mwendelezo wa vita ya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto mkoani Shinyanga, Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) imeanza kutoa mafunzo kwa wanachama wake ili kuwasaidia kutafiti, kuandika, kuandaa vipindi na kuelimisha jamii juu ya vitendo hivyo ili kuvitokomeza.
Mafunzo hayo ya siku moja yaliyobeba mada ya ‘Nafasi ya vyombo vya habari katika kumaliza ukatili dhidi ya wanawake na watoto’, yamefanyika leo Januari 14, 2020 mjini Shinyanga kwa ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT) ikiwa ni hatua za mwanzo za utekelezaji wa mradi wa miezi mitatu wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, John Tesha amesema kuwa waandishi wa habari mkoani humo wamesaidia kwa kiasi kikubwa kuelimisha, kutoa taarifa na kufichua vitendo hivyo, hivyo akawapongeza kwa juhudi kubwa wanazozifanya na kusisitiza kuwa mkoa huo umepiga hatua katika vita hiyo ikiwemo kuzindua mpango kazi wa miaka mitano.
Akitoa neno kwa wanachama wake, Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC), Patrick Mabula amebainisha kuwa tangu kuanzishwa kwake klabu hiyo imekuwa msaada mkubwa katika kukemea vitendo vya ukatili mkoani hapo.
Amesema kuwa Wanawake na watoto wamekuwa kwenye changamoto kubwa za vitendo vya kikatili, hivyo SPC kama jicho kubwa inayo nafasi ya kuifikia jamii na kusaidia kutoa elimu kumaliza tatizo hilo, huku akieleza kuwa SPC kwa ufadhili wa WFT watatekeleza mradi huo kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Januari 21 hadi Aprili 17, mwaka huu.
“Waandishi mtumie kalamu zenu vyema kuhakikisha mnaongeza ufahamu, kuibua na kukemea kwa namna yoyote vitendo hivi,” amesema.
Akitoa mafunzo kwa waandishi hao, Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, Angel Mwaipopo amesema hatua ya utoaji mafunzo kwa wanahabari ni sehemu ya Mpango kazi wa taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).
Angel amebainisha maeneo ya utekelezaji wa mpango huo kuwa ni kuimarisha uchumi wa kaya, kuhakikisha jamii inaendeleza mila chenye pekee, mazingira salama, malezi na kuimarisha familia, utekelezaji na usimamizi wa sheria, utoaji huduma kwa wahanga wa ukatili, mazingira salama shuleni na utaratibu, ufuatiliaji na tathmini.
Naye Mwakilishi kutoka Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Analyse Kaika akiwafunza wanahabari kuhusu sheria ya ulinzi wa mtoto na wanawake, amewahimiza kujikita katika kuzifahamu sheria na sera zinazowalinda watoto na wanawake ili kuandaa taarifa zenye na zinazosaidia kutokomeza vitendo vya ukatili.
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, Angel Mwaipopo akitoa mafunzo ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto mbele ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
Mwakilishi kutoka Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Analyse Kaika akitoa elimu ya sheria mbalimbali za ulinzi wa mtoto na wanawake katika mafunzo kwa wanahabari mkoa wa Shinyanga
Mwakilishi kutoka Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Analyse Kaika akitoa elimu ya sheria mbalimbali za ulinzi wa mtoto na wanawake katika mafunzo kwa wanahabari mkoa wa Shinyanga
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo
Viongozi wa SPC nao wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo
Waandishi wakichukua notisi kwenye kwenye mafunzo hayo
Waandishi wakisikiliza kwa umakini na kuchukua notisi kutoka kwenye mafunzo hayo
Wakiendelea kusikiliza kwa umakini
Waandishi wakipata elimu juu ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto
Mkufunzi Angel Mwaipopo akiendelea kutoa elimu kwa waandishi wa habari
Mafunzo yakiendelea kutolewa
Mafunzo yakiendelea
Waandishi wakisikiliza na kufuatilia kwa umakini mafunzo hayo
Elimu ikiendelea kutolewa
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
0 comments:
Post a Comment