Thursday, 21 January 2021

WAGANGA WA TIBA ASILI WATUMIE SUA NA WATAFITI WAKE KATIKA KUBORESHA BIDHAA ZILIZOPO NA KUANZISHA MPYA

...

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Utawala na Fedha Amandus Muhairwa akifungua kongamano kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda wakati akifungua Kongamano la siku moja la Watalaamu wa Tiba asili na kutoka maeneo mbalimbali nchini lililofanyika Chuoni kabla ya maonesho na uzinduzi wa jukwaa la ubunifu wa bidhaa za mimea dawa kwa maendeleo ya taifa lililoandaliwa na Mradi wa GRILI. 
Mratibu wa Utafiti na machapisho katika kurugenzi ya shahada za uzamili,utafiti,uhaulishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Japhet Kashaigiri akitoa salamu za kurugenzi yake kwenye kongamano hilo la wadau wa tiba asili nchini. 
Mtafiti Mkuu wa mradi wa GRILI Dkt. Faith Mabiki Akileza malengo ya mradi huo wa GRILI na malengo ya Kongamano hilo la wadau wa tiba asili nchini. 
Mkuu wa Ndaki ya Solomoni Mahlangu ya Sayansi na Elimu Dkt. Geofrey akitoa salamu za Ndaki yake na kuwakaribisha wageni hao Chuoni hapo. 
Wadau wa kongamano hilo ambao ni waganga wa tiba asili kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. 
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Utawala na Fedha Amandus Muhairwa (Katikati) akisikiliza maelezo toka kwa viongozi wa mradi, Prof. Samweli Kabote amabye ni Muwakilishi wa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na fedha (Wa kwanza Kushoto) Akifuatilia hotuba ya ufunguzi, wa kwanza Kushoto ni Dkt. Geofrey Kalugila Rasi wa ndaki ya Solomon Mahlangu ya sayansi na Elimu. 
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Utawala na Fedha Amandus Muhairwa akiangalia maonesho ya bidhaa mbalimbali za tiba asili zilizoletwa kwenye kongamano hilo kabla ya maonesho rasmi siku ya ijumaa. 
Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia ufunguzi wa Kongamono hilo na mada mbalimbali kutoka kwa wadasu wa tiba asili,Watafiti na watunga sera. 

***************************** 

Na: Calvin Gwabara – Morogoro. 
Waganga wa tiba asili nchini wametakiwa kuangalia kwa undani namna ya kutumia matokeo ya tafiti zinazofanywa na watafiti wa Chou Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Taasisi zingine ili kuboresha bidhaa zilizopo na kuanzisha bidhaa mpya ili kuendana na mahitaji ya jamii kwa wakati sahihi. 

Wito huo ulitolewa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Utawala na Fedha Prof. Amandus Muhairwa kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda wakati akifungua Kongamano la siku moja la Watalaamu wa Tiba asili na kutoka maeneo mbalimbali nchini lililofanyika Chuoni kabla ya maonesho na uzinduzi wa jukwaa la ubunifu wa bidhaa za mimea dawa kwa maendeleo ya taifa lililoandaliwa na Mradi wa GRILI. 

Prof. Mhairwa alisema kuwa njia hiyo ni muhimu sana hasa katika wakati huu ambao dunia inahangaika kutafuta chanjo na tiba ya ugonjwa wa COVID 19 ambapo dawa za mimea zimeonekana kufanya vizuri Zaidi kuliko za hospitalini, 

” Wanasayansi na waganga wa tiba ya asili sio kama vyama viwili vya upinzani, sisi tunafanya kazi kwa kutegemeana, sisi tunavitu tunavumbua kisayansi lakini pia kuna vitu vingine tunavifanyia utafiti vile ambavyo mmevianzisha nyinyi ili kuweza kupata udani Zaidi wa dawa mnazogundua kwahiyo hatupingi kazi zenu wala msituone kama vile maadui sisi tufanye kazi kwa pamoja kwa faida ya jamii na taifa letu” Alisisitiza Prof. Mhairwa. 

Alisema bidaa za mimea dawa zinakabiliwa na changamoto zinazohusiana na uzalishaji,uvunaji,utengenezaji,uuzaji na upatikanaji endelevu wa malighafi hivyo ili kupunguza changamoto hizo na kuzindoa kabisa kunahitajika utafiti Zaidi wa kisayansi,ubunifu Zaidi katika masoko,uzingatiaji wa hali ya juu wa vigezo vya ubora vinavyotakiwa na kufuata taratibu za biashara zenye tija. 

Lakini pia aliwataka Wataalamu hao wa Tiba asili kuangalia masuala ya kisera yanayoleta changamoto katika kuhaulisha teknolojia hizi ili ziweze kutumika kibiashara na kuanzisha viwanda vya uzalishaji wa mimea dawa na hasa katika kipindi hiki ambapo sera ya serikali ni kusukuma uanzishwaji wa viwanda kwenye sekta hii. 

Naibu Makamu huyo wa Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha aliwahakikishia kuwa SUA na hasa kurugenzi ya uzamili,Utafiti,Uhaulishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu kwa kushirikiana na serikali wataendelea kuwa nao bega kwa bega kwa kusaidia jitihada za wadau wote kwenye sekta hii katika kuboresha tafiti za oaina hii kwa kadri mazingira yatakavyoruhusu. 

Akitoa salamu kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua kongamano hilo Mratibu wa Utafiti na machapisho katika kurugenzi ya shahada za uzamili,utafiti,uhaulishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Japhet Kashaigiri alisema kuwa kurugenzi hiyo na vitengo vingne vya SUA vimekuwa na utaratibu wa kuandaa makongamano ya aina hiyo ili kujaribu kuboresha biashara za mazao ya Kilimo,Ufugaji na Misitu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika sekta hizo. 

“Katika makongamano haya SUA imekuwa ikishirikisha wasimamizi na wakaguziwa ubora wa biashara hizi pamoja na watunga sera kwa ujumla na utaratibu huu umeongeza mchango mkubwa wa chou chetu katika kutatua changamoto mbalimbali na kuboresha biashara za mazao nah ii ni muhimu hasa katika awamu hii ya serikali ya tano ambayo mwelekeo wake ni kuwa uchumi wa viwanda. 

Prof. Kashaigili alisema Vyuo Vikuu kote duniani ni vitovu vya maendeleo ya kitaaluma na Tafiti mbalimbali na kwa muktadha huo kurugenzi ya uzamili kupitia kitengo chake cha uhaulishaji wa teknolojia pamoja na mradi wa GRILI zimeona ni vyema kutumia uzoefu wake wa ndani na kwa kushirikiana na wadau wengine kuandaa kongamano hili hapa SUA ili kuwaleta wadau wote pamoja na kujadili namna ya kukuza uelewa na kutatua changamoto hizo. 

Akileza malengo ya mradi huo wa GRILI na malengo ya Kongamano hilo Mtafiti mkuu wa mradi huo Dkt. Faith Mabiki amesema Utekelezaji wa mradi huu ulianza mwaka 2018 ukiwa na lengo la kuchangia katika kuongeza ubora wa bidhaa za miti dawa ili kuboresha Maisha ya watengenezaji,afya za watumiaji na kuchangia katika pato la taifa. 

Dkt. Mabiki alisema ili kufikia malengo hayo ya muda mrefu mradi huo unajenga uwezo wa kitafiti wa kitafiti kwa wanafunzi wa shahada za uzamivu 5 na shahada za uzamili 2 katika maeno muhimu ya kemikali,usugu wa dawa na masoko na unategemea kutoa matokeo ya kitafiti yatakayo tumika na wadau muhimu wa kuboresha biadhaa hizi. 

“Kongamano hili la kitaalamu la wadau likiwa ni moja ya shughuli za uzinduzi wa Jukwaa la ubunifu wa bidhaa za mimea dawa kwa maendeleo ya taifa litajikita Zaidi kwenye kujadili Uboredhaji wa uzalishaji,uchakataji,ufungsdhsji na uuzaji wa bidhaa zinazotokana na mimea dawa hapa Tanzania na namna ya kutatua changamoto hizo” Alisema Dkt. Mabiki. 

Kwa upande wake Mkuu wa Ndaki ya Solomoni Mahlangu ya Sayansi na Elimu Dkt. Geofrey alisema kwa upande wa utafiti ndaki hiyo ni ya pekee inayotoa shahada ya uzamili ambazo zinajikita moja kwa moja katika utafiti wa mazao ya mimea dawa ambayo mojawapo inahusika katika tukio hili na ina miradi Zaidi ya tisa ambayo kwa namna moja au nyingine zinagusa bidhaa hizi za mimea dawa. 

“Kwa sababu hiyo tunategemea kuchangia juhudi za SUA na Taifa katika kuongeza ubora wa bidhaa hizi ili zipate Masoko” Alisisitiza Dkt. Kalugila. 

Pia Dkt. Geofrey Kalugila aliwashukuru wadau hao kutoka maeneo yote nchini kufiki akushiriki kwenye kongamano hilo,maonesho na uzinduzi wa Jukwaa la ubunifu na kuwataka watumia siku chache watakazokuwa SUA kujifunza na kujionea mambo mbalimbali ya kistoria kwenye kampasi hiyo ambayo ilikuwa kambi ya wapigania uhuru wa Afrika kusini. 

Kongamano hilo litafuatiwa na Maonesho makubwa ya Tiba asili na bidhaa zake litakalofanyika kwenye viwanja vya soko kuu la mkoa wa Morogoro tarehe 22/01/2021 na baada siku ya jumamosi kutakuwa na uzinduzi wa Jukwaa la ubunifu wa bidhaa za tiba asili litakalofanyika kwenye kampasi ya Solomon Mahlangu Mazumbu tarehe 23/01/2021 zilizoandaliwa na Mradi wa GRILi.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger