Thursday, 14 January 2021

Rais Wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi Na Makamu Wake Wa Kwanza Maalim Seif Shariff Hamad Wamtembelea Rais Dkt. Magufuli Kijijini Chato Leo

...


 Rais Dkt John Magufuli ameahidi kushirikiana na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuhakikisha Zanzibar inaendelea kuwa amani na inaendelea kukua kiuchumi.

Dkt Magufuli ametoa kauli hiyo wilayani Chato mkoani Geita akiwa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapibduzi Dkt Hussein Mwinyi pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Sharif Hamad, waliomtembelea nyumbani kwake na kufanya nae mazungumzo.

Amesema katika siku za mwanzo za uongozi wao, Viongozi hao wamefanya mambo makubwa yanayoashiria mwanga wa maendeleo Visiwani Zanzibar.

Rais Magufuli amewataka Viongozi hao kuendelea kushirikiana katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kuendelea kuhubiri amami miongoni  kwa Wakazi wa Zanzibar na Watanzania wote, kwani amani ndio msingi wa maendeleo.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger