Picha ya kitanda
Na Mgongo Kaitira - Mwananchi
Mtu mmoja ambaye jina lake halijatambulika amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni akiwa na mwanamke anayehisiwa kuwa ni mpenzi wake.
Tukio hilo limetokea Januari 18, 2021 katika nyumba ya kulala wageni ya Fimbo Lodge iliyopo mtaa wa Kilimahewa Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.
Mmiliki wa nyumba hiyo, Christopher Lyang’ombe akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Januari 21, 2021 amekiri kutokea kwa tukio hilo akisisitiza watafutwe polisi kwa kuwa ndio wanaoendelea na uchunguzi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanamshikilia kwa mahojiano mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa) anayedaiwa kuwa mtu wa karibu wa marehemu na ndiyo alikuwa naye katika nyumba hiyo.
“Mtu anayetuhumiwa inadaiwa ni mtu wake wa siku nyingi tunamhoji tu ila upo ushahidi wa awali unaoonyesha alikuwa na matatizo ya presha,” amesema Muliro.
Tukio hilo limetokea ikiwa zimepita siku tano tangu kutokea kwa tukio kama hilo ambapo mkazi wa Goba jijini Dar es Salaam, David Makerege (80) alifariki dunia katika hoteli ya Mbezi Garden alipokuwa na Neema Kibaya (33).
CHANZO - MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment