Kikosi cha timu ya Mtwivila city (Ifuenga united) kilichofanikiwa kuingia fainali ya Asas super league
Na Fredy Mgunda na Denis Mlowe ,Iringa.
TIMU ya soka ya Mtwivila city (Ifuenga united) imefanikiwa kuingia fainali ya ligi soka daraja la tatu mkoa wa Iringa kwa baada ya kuifunga timu ya soka Irole fc mabao 2 - 1 katika mchezo mkali wa nusu fainali ya pili iliyochezwa kwenye uwanja wa Mkwawa.
Hivyo kutokana matokeo hayo timu ya soka ya Ifuenga United watakutana na Ivambinungu fc siku ya jumapili katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Samora.
Timu ya Ivambinungu Fc ilikuwa timu ya kwanza kutangulia kwenda fainali baada ya kuwafunga timu ya Kidamali Fc kwa jumla ya magoli 3-1 na kuifanya timu hiyo kufika fainali baada ya kushinda nusu fainali zote mbili zilizopigwa katika viwanja vyote viwili vya nyumbani na ugenini.
Nayo Timu ya Mtwivila city (Ifuenga united) imeingia fainali baada ya kuifunga timu ngumu ya Irole Fc kwa jumla ya goli mbili moja baada ya michezo yote miwili iliyochezwa nyumbani na ugenini.
Akizungunza mara baada ya mchezo wa nusu fainali ya pili kocha wa timu ya Ifuenga Edger Nzelu alisema kuwa timu hiyo imejipanga vilivyo kuhakikisha wanashinda fainali kwa kuwa mchezo huo muhimu ambao kwa namna yoyote ile lazima washinde kwenda katika ngazi ya kanda.
Nzelu alisema kuwa baada ya kushinda mchezo huo mgumu wa nusu fainali ana uhakika wa kushinda mchezo wa fainali yenyewe kwa kuwa timu hiyo ya Irole Fc ndio ilikuwa kikwazo kwao.
Aliwataka mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuisapoti timu hiyo ili kuipa nguvu kuhakikisha kwenye fainali na kwenda mbele kwenye mashindano ngazi nyingine
Naye mfadhili wa timu hiyo Joseph Kilienyi alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo wa fainali na kuchukua kombe hilo.
Alisema kuwa timu ya Ivambinungu Fc ni timu nzuri lakini wao wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo huo muhimu kwao kwa kuwa wanataka kwenda kanda na kuhakikisha timu hiyo inafika katika madaraja ya juu na hatimaye kufika ligi kuu Tanzania Nara.
Timu ya Mtwivila city (Ifuenga) imejipanga kwa kila kitu hivyo wakiwa mabingwa wa mkoa watahakikisha timu hiyo hairudi nyuma tena kwenye ligi ya mkoa wa Iringa tena.
Bingwa wa ligi hiyo iliyojizoelea umaarufu nchini kutokana na udhamini wa kampuni ya maziwa ya Asas ataondoka na sh milioni 2.5 huku mshindi wa pili akichukua milioni 1.5 na mshindi wa tatu ataibuka na laki 750000 baada ya zawadi kuongezwa kwa washindi.
0 comments:
Post a Comment