Monday, 18 January 2021

MCHUNGAJI WA KANISA LA 'YESU NAKUPENDA UMEOKOKA' AUAWA KWA KUCHOMWA KISU

...

Picha haihusiani na habari hapa chini

Na Rose Jacob - Mwanza
Mchungai wa Kanisa la Yesu Nakupenda Umeokoka, Beneth Karange (66) na binti yake Renatha Beneth (42), wilayani Nyamagana, jijini Mwanza wameuawa kikatili kwa kuchomwa kisu na mtoto wake wa kiume ambaye naye alifariki baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira.

Anayedaiwa kutekeleza mauaji hayo ni kijana wake wa kiume, Richmond Beneth, ambaye naye alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali ya Sekouture, kutokana na kupigwa na wananchi wenye hasira.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Murilo Jumanne, alisema  tukio hilo limetoke juzi saa tisa alasiri ambapo Richmond (32), alikuwa akisoma Chuo Kikuu cha Kampala kilichopo jijini Dar es Salaam.

Kamanda Muliro alisema, kijana huyo ambaye naye aliuawa, aliwachoma kisu baba na dada yake sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha vifo vyao papo hapo.

Muliro alisema kijana huyo aliyesababisha mauaji hayo, alirudi nyumbani kutoka chuoni kwa kukosa ada.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger