Wizara ya Viwanda,na Biashara kupitia taasisi yake ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inawakaribisha Watanzania wote kutembelea Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yatakayoanza tarehe 3 hadi 9 Desemba, 2020. Uanzishwaji wa Maonesho haya yalilenga kuhakikisha Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda unakuwa na matokeo chanya katika uchumi na yanayoonekana.
Maonesho haya yanalenga kujenga jukwaa kwa Wadau wa Sekta ya Viwanda kupata fursa ya kujadiliana, kubadilishana uzoefu na kutangaza fursa zilizopo katika Sekta hiyo. Aidha, Maonesho hayo hususan, yanalenga kutoa fursa zifuatazo:-
i. Kuvitambua viwanda vya Tanzania pamoja na bidhaa zinazozalishwa nchini ili Watanzania wazitambue na kupenda kuzitumia;
ii.Kuhamasisha Watanzania kutumia bidhaa na huduma zinazozalishwa hapa nchini;
iii.Kuwaunganisha wenye Viwanda na Wazalishaji mbalimbali wa Malighafi na huduma zingine zinazotumika viwandani; na
iv. Kuwaunganisha wenye Viwanda na Wasambazaji wa teknolojia za viwanda.
Kauli Mbiu ya Maonesho haya ni “Tumia Bidhaa za Tanzania, Jenga Tanzania” ikiwa ni kuhamasisha Watanzania waendelee kupenda, kununua na kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya Tanzania kwa lengo la kuchochea uzalishaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi ili kukuza soko la ndani na hatimaye kuiwezesha Tanzania ambayo imeingia katika Uchumi wa Kati.
Pia, Maonesho haya yataenda sambamba na matukio mbali mbali kama ifuatavyo:-
Tarehe 5 Desemba, 2020 kutakuwa na Mkutano kati ya Wizara ya Viwanda na Biashara, Wamiliki wa Viwanda nchini na Taasisi za Uthibiti. Mkutano huu utalenga kutatua changamoto zinazowakabili wamiliki wa viwanda katika uendeshaji wa shughuli za uzalishaji wa bidhaa nchini.
Tarehe 6 Desemba, 2020 kutakuwa na Bonanza la Maziwa litakalo husisha matembezi ya Afya (Jogging) na michezo mbalimbali. Lengo la kuwa na Bonanza la Maziwa ni kuhamasisha unywaji wa maziwa yanayozalishwa na Viwanda vya Tanzania. Washiriki na Watembeleaji wa Maonesho watapata kuvitambua na kunywa maziwa kutoka viwanda vyetu vya ndani. Zoezi hili linahamasisha matumizi ya bidhaa za maziwa yanayozalishwa nchini.
Tarehe 7 Desemba, 2020 kutakuwa na kongamano la biashara lenye kuelezea fursa za biashara katika nchi za Dubai, Falme za Kiarabu na Kuwait litakaloenda sambamba na mikutano ya biashara ya ana kwa ana (B2B Meeting) na
Huduma ya kliniki ya biashara itatolewa kuanzia tarehe 3 hadi 9 Desemba, 2020 ambapo taasisi zinazosimamia mnyororo wa biashara nchini zitasikiliza na kutatua kero/changamoto za wazalishaji wa bidhaa za Tanzania ana kwa ana
Mabanda ya yatafunguliwa saa 4 kamili asubuhi hadi saa 12 Jioni, hakuna kiingilio kwa watembeleaji. Wote mnakaribishwa
Imetolewa na;
Theresa Chilambo
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
0 comments:
Post a Comment