Picha ya jogoo
Wananchi wa kijiji cha Luanda Kaunti ya Vihiga nchini Kenya wameachwa na mshangao mkubwa na kuchanganyikiwa baada ya jogoo anayedaiwa kuibwa katika Kaunti nyingine kukataa kuuzwa licha ya bei yake nafuu.
Mwizi aliyekuwa amemleta jogoo wa kuiba katika soko la Luanda alijikuta katika wakati mgumu baada ya kutaka kumuuza jogoo huyo.
Jogoo alikataa kuuzwa hata baada ya mnunuzi kupatikana wa bei nafuu ambapo hali hiyo iliwafanya watu kumhoji mwizi huyo alikomtoa kuku huyo.
Mdakuzi wetu aliyeshuhudia sinema hiyo anasema kuwa, yeye pia alichanganyikiwa kama walivyochanganyikiwa wengine, baada ya kugundua kuwa, Jogoo huyo kutoka Kaunti ya Siaya, alimkatalia mwizi (kwa jina William) kila mara alipotaka kumuuza.
Tukio hilo lilitokea na kujirudia mara 4 hadi watu waliokuwa sokoni walipoanza kushuku na kuamua kumkabili mtu huyo.
Walimhoji kumhusu jogoo huyo ambaye bei yake ilikuwa KSh 800, bei ya kutupa.
Wafanyabiashara katika soko hilo, walimhoji William na kutaka kufahamu ni kwa nini jogoo huyo alikuwa akionyesha tabia isiyokuwa ya kawaida.
Kwa kuwa soko hilo lipo mpakani, inadaiwa mwenye kuku huyo alikuwa amefika katika soko hilo na alikuwa akimsaka kuku huyo.
Baada ya muda wakimhoji, kumbe taarifa ilikuwa imemfikia mwenye jogoo ambaye alifika na hatimaye kumtambua kuku wake aliyekuwa ametoweka.
Katika hali ya kushangaza sana, mtu huyo alisema amefanya urafiki mkubwa na mifugo wake, na kwamba ni vigumu mtu yeyote kumwibia.
Aliondoka na kuku wake huku husika wa wizi akiponea kichapo kwa kupigwa kitutu na umma.
Hata hivyo, ilidaiwa mwenye jogoo huyo ni mganga ambaye nguvu zake na dawa zilichangia kuku huyo kukataa kununuliwa kwani sio hali ya kawaida.
Chanzo - Tuko News blog
0 comments:
Post a Comment